June 14, 2018


Tottenham wameipa Aston Villa ofa ya pauni milioni 15 kwa kiungo wake wa kati Jack Grealish, lakini Chelsea, Fulham na Leicester pia wanamtaka mchezaji huyo wa maiaka 22. (Sky Sports)

Burnley wanataka kuwasaini mlinzi wa England Craig Dawson, 28, na mshambuliaji wa England Jay Rodriguez, 28, kutoka West Brom kwa pauni milioni 28 kwa pamoja. (Mail)

Arsenal wako kwenye mazungumzo na Bayern Leverkusen kumsaini kipa mjerumani Bernd Leno, 26. (Sky Sports)

Arsenal wanakaribia kutumia pauni milioni 50 kununua wachezaji wakiwemo kiungo wa kati wa Sampdoria raia wa Uruguay Lucas Torreira, 22, na beki wa Borussia Dortmund mgiriki Sokratis Papastathopoulos, 30. (Evening Standard)


Mshambuliaji wa Manchester City Mhispania Brahim Diaz, 18, anatafutwa na meneja wa West Ham Manuel Pellegrini kwa mkopo wa muda mrefu. (Sun)

Mlinzi wa Ujerumani Jerome Boateng, 29, ambaye anawinda na Manchester United, ataruhusiwa kuondoka Beyern Munich kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa klabu, Karl-Heinz Rummenigge. (Manchester Evening News)

Mlinzi wa Newcastle raia wa Congo Chancel Mbemba, 23, amekubali mkataba wa miaka minne na Porto wa thamani ya pauni milioni 8. (Mirror)


Meneja wa Derby Frank Lampard anamtaka mchezaji wa Chelsea wa miaka 20 raia wa England Jay Dasilva. (Talksport)

Mshambuliji wa Liverpool Sadio Mane, 26, anasisitiza kuwa yuko na furaha huko Liverpool baada ya uvumi kuwa anataka kuhamia Real Madrid. (BT Sport)


Kocha wa Jeventus Massimiliano Allegri, 50, anasema alizungumziwa na Real Madrid kuhusu kuchukua mahala pake Zinedine Zidane - lakini akakataa. (The Sun)

Kutoka BBC


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic