June 22, 2018


Klabu ya Mtibwa Sugar imeingia mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji kutoka Kagera Sugar, Jaffar Kibaya.

Kibaya ambaye aliwahi kuichezea Mtibwa kabla ya kutimkia Kagera, amejiunga na wakata miwa hao wa Manungu kwa ajili ya kuboresha safu yao ya ushambuliaji.

Usajili hao umekuja ambapo Mtibwa inajiandaa kushiriki michuano ya kimataifa (CAF Confederation CUP) baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la Azam Sports Federation CUP.

Mbali na mashindano ya CAF, Mtibwa wanakiandaa kikosi chao vizuri kuelekea michuano ya Ligi Kuu Bara katika msimu wa 2018/19.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic