March 7, 2018



Na George Mganga

Dak ya 1, Mechi imeanza katika Uwanja wa taifa

Dak ya 2, Masry wanarusha mpira kuelekea langoni mwa Simba, inapigwa krosi kali, Manula anautoa, kona

Dak ya 3, Okwi anakwenda mpira pembezoni kuli mwa Uwanja, anapiga krosi lakini unaokolewa hapa

Dak ya 4, Masry wanaanza sasa, unapigwa mreefu mpaka kwa kipa wa Simba, Manula anaudaka

Dak ya 5, Mpira umesimama kwa muda kufuatia mchezaji wa Masry kuumia, ameshanyanyuka sasa, mpira unaendelea

Dak ya 6, Hatari katika lango la Masry, Nyoni anapiga krosi, kona, Kichuya anapiga tena kipa anaokoa na kuutoa nje, kona ya pili

Dak ya 8, Penatiiii, Simba wanapata penati baada ya beki wa Masry kuushika mpira

Dak ya 9, Bocco anapigaaa, gooooooooooooooli

Dak ya 11, Gooooooli, Masry wanasawazisha hapa ni 1-1, mfungaji ni Mohammed Gomaa 

Dak ya 12, Simba wanapasiana sasa eneo la nyuma, Kapombe anampasia Kapombe, Kapombe kwake Erasto Nyoni

Dak ya 15, Gyan anachezewa faulo wakati akipandisha mashambalizi, mpira unapigwa kuelekea lango la Masry

Dak ya 16, Mpira wanao Simba, anapasiwa Kwasi lakini mpira unatoka nje

Dak ya 18, Mpira anao Kwasi saa, kwake Bocco lakini unaokolewa, Simba wanauchukua tena kwake Okwi, mabeki wa Masry wanambana na kumnyang'anya mpira

Dak ya 19, Kapombe sasa, kwake Kotei, Boco kwake Kichuya, wanapasiana sasa anauchukua Okwi, lakini Masry wanauchukua tena

Dak ya 21, Mpira umesimama, mchezaji wa Masry kaumia

Dak ya 22, Mpira ushaanza tena, Simba wanautoa na unarushwa kuelekea langoni mwa Simba

Dak ya 23, Masry wanarusha tena mpira kuelekea langoni mwa Simba baada ya kutolewa nje

Dak ya 24, Penatiii, inapigwa kuelekea langoni mwa Simba baada ya Kotei kuunawa

Dak ya 25, Gooooo, Masry wanafunga la pili, penati ya Ahmed inaingia kimiani

Dak ya 27, Mchezaji wa Masry amedondoka hapa, Masry wako mbele kwa mabao 2-1

Dak ya 29, Faulo inatokea hapa baada ya Kotei kudondoshwa, Kapombe sasa anamtafuta Okwi lakini mpira unaokolewa na wapinzani

Dak ya 32, Faulo inapigwa kueleka Masry

Dak ya 33, Mchezaji wa Masry kaumia, mpira umesimama

Dak ya 35, Mpira bado umesimama

Dak ya 36, Mpira umeshaanza, sasa Nyoni kwake Kichuya, unapigwa kwake Kotei, faulo

Dak ya 38, Okwi anapigaaa, kipa anadaka

Dak ya 39, Boccooo, Mwamuzi anapuliza kipyeng, ni offside

Dak ya 40, Matokeo bado ni 2-1

Dak ya 41, Hatari katika lango la Simba lakini mabeki wanaokoa, mpira unapigwa mbele na mabeki wa Masry wanatoa, unarushwa kuelekea Masry

Dak ya 42, Simba wanapata kona, inapigwa, hatarii, lakini mpira unatoka nje, ni goli kiki

Dak ya 44, Simba wamapunguza makali, Masry wanalijia lango la Simba

Dak ya 45, Dakika 3 zinaongezwa kuelekea mapumziko

Dak ya 47, Masry wanatumia muda mwingi kupoteza muda

Mpira ni mapumziko sasa, Simba 1-2 Masry

Dak ya 45 kipindi cha pili sasa, anapiga mbele huku lakini mchezaji wa Masry anachezewa faulo

Dak ya 47, unapigwa kuelekea lango la Simba, Manula anadaka, anaanza taratibu na mabeki zake

Dak ya 47, faulo inapigwa kwenda lango la Masry

Dal ya 48, Masry wanarusha mpira,

Dak ya 52, Kwasi ameumia, mpira umesimama

Dak ya 53, Kwasi anaumia tena mapema baada ya mpira kuanza

Dak ya 54, Masry wanarusha karibu na eneo la Simba, unarushwa, hatariii, shuti kali na mshambuliaji wa Masry linakwenda nje

Dak ya 55, Hatariiii katika lango la Masry, mpira unapita na kwenda nje

Dak ya 56, Kapombe anapoteza mpira kizembe, Masry wanachukua, Nyoni anapewa kadi ya njano baada ya kucheza madhambi

Dak ya 60, Free Kiki inapigwa kuelekea Masry, Kichuya anapiga, anapigaaa, kipa anadaka

Dak ya 62, Goli kiki, Simba wanaanza, Asante kwake Mkude, mpira unatoka nje, Simba wanarusha

Dak ya 64, Mkude sasa anamiliki mpira, anachezewa faulo, Simba wanaanza

Dak ya 64, Kotei anapasi kwake Gyan, Gyan kwake Okwi, Okwiiii inagonga mwamba, hatari

Dak ya 67 sasa, Kwasi anao mpira, unatolewa nje, unarushwa kuelekea kwa wapinzani

Dak ya 68, Gyaaan, mpira unakwenda, Simba wameanza kuamka sasa

Dak ya 69, Simba Sc 1-2 Al Masry SC

Dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Taifa, matokeo ni 29

Dak ya 70, Simba wameamka, Kichuya, hatarii, kona, inapigwa lakini unatoka nje, goli kiki

Dak ya 72, penatiiii, Simba wanapata penati ya pili

Dak ya 73, Gooooooli, Okwi anafunga bao la pili, sasa ni 2-2

Updates Mpira umesimama kwa muda, taa zimezima Uwanjani

Full Time, mpira umemalizika uwanja wa taifa, Simba 2-2 A Masry SC

24 COMMENTS:

  1. BHAHAHAHAHAAAA, SIMBA INAKALIA DUDU

    ReplyDelete
  2. Mpira ni Dk. 90 na hao Waarabu wanavyopoteza muda hauoni au?

    ReplyDelete
  3. Unafananisha na mpira wa jana, watu tumekosa raha kabisa

    ReplyDelete
  4. Unaweza kufananisha na mpira wa jana? Watu tumekosa raha kabisa.

    ReplyDelete
  5. Nayakumbuka ya Haras al Hudood!! Simba alipigwa nje ndani. Matatizo yetu ni kuchezea mpira kwenye media na kukariri historia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio kweli, simba walishinda 2-1 dsm. Usipotoshe umma

      Delete
  6. Haras al hudoud alifungwa 2-1 na Simba. Tarehe 26 April 2010.Wacha uongo au umeanza juzi kuwa shabiki.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Halafu Simba wakaendelea na mashindano!! Toa matokeo kamili

      Delete
    2. Wacha ujinga.Ulichosema ndio tulichopinga kwamba Simba alifungwa ndani nje. Wakati ni uongo.

      Delete
    3. Washamba utawajua kwa hasira

      Delete
  7. Hebu tuendelee kufuatilia mechi, maneno ya nini?

    ReplyDelete
  8. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  9. Bado muda. Matokeo yanaweza kubadilika.

    ReplyDelete
  10. Ila hizi kosakosa kwa nini hawakuzifanya mapema?

    ReplyDelete
  11. Mungu ibariki Simba iweze kutupatia raha watanzania

    ReplyDelete
  12. Mpira vijana wetu wa Simba wanacheza jamani. Unapokutana na Al Masry sio wale wa Botwana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Waambie hao viwete. Unafungwa na timu kutoka Botswana halafu unaongea mbele ya wanaume.

      Delete
  13. Umeona mpira wa kimataifa eeeeeeeeeeeeehhhhhheeeeeeeeee

    ReplyDelete
  14. Sasa taa kuzimika LUKU imeisha au mitambo ya TANESCO?

    ReplyDelete
  15. Am Yanga Damu but leo my prayers was for Simba@ 100%.Jamani tufunze kuwa watanzania Nenda Misri HAKUNA NARUDIA HAKUNA MWAARABU ATASHANGILIA SIMBA BUT LEO BAAZI YA WATANZANIA ETI MASHABI WAYANGA WAMEIPA SUPPORT ALMASRY KWAKUISHANGILIA!!! Jamani are we rational or irrational animals? Nenda Botswana wiki ijayo HAKUNA MSWANA NARUDIA HAKUNA MSWANA ATAISHANGILIA YANGA!! Hivi yanga ama simba inapoingia kwenye hatua ya makundi mnajua ni nani atafaidika?? Watafiadika vijana wenzetu, wazee wetu, wadogo zetu etc etc !!! Hivi kwa mfano sasa tp mazembe ni nembo ya drc ! Hivi mnafikiri mafanikio hayo ni ya tp mazembe tu ama ni nchi kwa ujumla ya drc?? JAMANI TUACHE UJINGA AMBAO UNAFANANA NA KUAKISI UMASKINI NA ILLITERATE YA HALI JUU! lets think litle bit outside the box.

    ReplyDelete
  16. Sare ya 2-2 ugenin mwaraabu hesabu amesonga mbele krbun tena mchome mahindi kwny msimbaz mkisubiri mwakani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic