June 13, 2018


Shirikisho la Soka nchini Spain chini ya Rais wake, Luis Rubiales, umesema upo kwenye mipango ya kumfukuza kazi Kocha Mkuu wa timu ya taifa hilo, Julen Lopetegui.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya kutangazwa na klabu ya Real Madrid jana kuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo ili kuchukua nafasi ya Mfaransa, Zinedine Zidane.

Taarifa zinaeleza kuwa kwa Rubiales ameitisha kikako cha dharura kwa ajili ya kujadili juu ya uamuzi wa kocha huyo kutimkia Real Madrid akisema anaweza akasababisha ubaguzi katika uteuzi wa wachezaji katika timu ya taifa.

Imeelezwa Lopetegui baada ya kujiunga na Real Madrid kuwa anaweza akashindwa kuwapa nafasi kubwa wachezaji wa FC. Barcelona na Real Madrid ambao ni wapinzani wakubwa wa mabingwa hao wa taji la UEFA kwa msimu uliomalizika hivi karibuni.

Rais Rubiales amefunguka kuwa ili kuepuka suala hilo kujitokeza amebidi kuitisha kikako na viongozi wake wa shirikisho ili kuamua kama Lopetegui anaweza akafukuzwa kazi kabla ya michuano ya Kombe la Dunia kuanza na mtu mwingine kupewa nafasi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic