SANGA AFUNGUKA HAYA KUHUSIANA NA KUGOMBEA UENYEKITI YANGA
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga, amefunguka kuhusiana na kugombea nafasi ya uongozi ndani ya klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Radio EFM, Sanga ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania, amekaa pembeni kwa muda mrefu nje ya wadhifa huo baada ya kuteuliwa na TFF kushika wadhifa mwingine wa Uenyekiti.
Wakati Yanga ikijipanga kuelekea uchaguzi mkuu wa kumtafuta Mwenyekiti wake baada ya Yusuph Manji kujiuzulu nafasi hiyo, Sanga amesema kuwa hana mpango wa kugombea nafasi hiyo.
Kiongozi huyo ambaye pia yupo TFF ameeleza kuwa yeye atabakia kuwa mwanachama ndani ya Yanga huku akitoa kheri zake kuelekea uchaguzi huo.
Hivi karibuni BMT iliitaka Yanga kufanya uchaguzi kujana nafasi hiyo ambayo imekaa wazi kwa muda mrefu.
Mficha uchi hazai..
ReplyDelete..tatizo ni kubwa lakini wanachama hawashirikishwi katika kutatua....sasa ngome inaendelea kumeguka kocha, viongozi, wachezaji kutosajili...
Kumbukeni bado kuna mashindano ya CAF mechi kama nne zimebaki....lazima mfanye uchaguzi ndani ya wiki mbili, pia mteue benchi la ufundi la muda, na msajili wachezaji sio kuongea tu...lugha kama hizi hazitakiwi.
..tuko kwenye mpango, tunategemea, tunatafuta, tunaandika barua.....huu ni uzembe....wengine wanatoa pesa wanachukua mchezaji!
Mkutano wa Yanga ni Jumapili kwanini idara ya katibu mkuu haijaweka promotion kwenye vyombo vya habari mitandao ya jamii kuhamasisha wanachama wa Yanga nchi nzima wakiwemo wa mikoani kuhudhuria.....Simba wapo vizuri katika kupromote vitu na mambo yao.....kupromote haihitaji fedha lakini ni ubunifu tu.....mkutano ni jumapili na ni wa maana sana lakini magazeti na mitandao iko too quiet WHY MKWASA???
ReplyDelete