June 5, 2018


Wakati vuguvugu la usajili kwa wachezaji wa Ligi Kuu Bara likiendelea hivi sasa, Katibu Mkuu klabu ya Yanga, Boniface Mkwasa, amefunguka kwa kusema timu zinazosajili hivi sasa zinakiuka kanuni.

Kwa mujibu wa Radio One, Mkwasa ameeleza kuwa klabu zinazosajili zinaenda kinyume na taratibu kwasababu dirisha rasmi la usajili halijafunguliwa.

Katibu huyo amesema hayo kufuatia timu mbalimbali haswa za ligi kuu kuendelea na usajili wa wachezaji ambao wamekuwa wakisaini mikataba ya awali.

"Unajua klabu zinazosajili hivi sasa zinaenda kinyume na utaratibu wa usajili, na hii yote ni kwasababu dirisha bado halijafunguliwa" alisema.

Mpaka sasa Yaanga haijaweka wazi ni wachezaji gani imewasajili zaidi ya kusikia tetesi zinazodai tayari imeshamalizana na mchezaji wake wa zamani, Mrisho Khalfan Ngassa.

7 COMMENTS:

  1. Walipomuiba khasan kessy kutoka simba na wengineo wengi mbona hatukumuona kufunua mdomo wake kukemea? Aache unafiki na wala hapaswi kuhangaikia ya nje ya nyumba yake ashughulikie ule uozo uliokuwepo pale Yanaga kwanza.

    ReplyDelete
  2. Bora eende TFF ukawafundishe sheria kuliko kuropokwa kusio na maana. Jaribuni kumkabidhi Akili Mali muone mambo atavoyatengeza

    ReplyDelete
  3. Kwani yeye ni kiongozi au msemaji wa TFF?..Aache kutapatapa , apambane na hali yake

    ReplyDelete
  4. Mficha uchi hazai..
    ..tatizo ni kubwa lakini wanachama hawashirikishwi katika kutatua....sasa ngome inaendelea kumeguka kocha, viongozi, wachezaji kutosajili...
    Kumbukeni bado kuna mashindano ya CAF mechi kama nne zimebaki....lazima mfanye uchaguzi ndani ya wiki mbili, pia mteue benchi la ufundi la muda, na msajili wachezaji sio kuongea tu...lugha kama hizi hazitakiwi.
    ..tuko kwenye mpango, tunategemea, tunatafuta, tunaandika barua.....huu ni uzembe....wengine wanatoa pesa wanachukua mchezaji!

    ReplyDelete
  5. Mnahitaji kuwaacha wachezaji wabovu km mwashiuya, mahadhi, Tambwe,Kakolanya, Youthe, Ngoma yule mkongo aliyesajiliwa akala fedha halafu akakimbia na martin. Kisha kusajili Allan Wanga, Marcell Koupko, Pascal Wawa, Ley Vuy Matampi, Benedict Tinoco, Ditram Nchimbi, Boniface Maganga, Nurdin Chona, Hassan Kabunda na Peter Mapunda

    Ushauri tu

    ReplyDelete
  6. Mnahitaji kuwaacha wachezaji wabovu km mwashiuya, mahadhi, Tambwe,Kakolanya, Youthe, Ngoma yule mkongo aliyesajiliwa akala fedha halafu akakimbia na martin. Kisha kusajili Allan Wanga, Marcell Koupko, Pascal Wawa, Ley Vuy Matampi, Benedict Tinoco, Ditram Nchimbi, Boniface Maganga, Nurdin Chona, Hassan Kabunda na Peter Mapunda

    Ushauri tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic