June 2, 2018


Na George Mganga

Vita iliyosubiriwa kwa hamu jijini Arusha na wadau wengi wa soka imefika rasmi ambapo Singida United na Mtibwa zinakutana leo katika mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho atakayeiwakilisha Tanzania Kimataifa.

Mechi hiyo itaweka historia ya aina yake kuchezwa jijini humo kwani itakuwa ni ya kwanza tangu kuanzishwa kwa michuano hii nchini Tanzania.

Kuelekea mechi hiyo, makocha wa timu zote mbili wameahidi kupigania ushindi ili kupata nafasi adhimu kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kuhusiana na suala la Mtibwa Sugar iliyowahi kufungiwa kushiriki michuano ya kimataifa mwaka 2000 na CAF baada ya kushindwa kusafirisha timu sababu ya ukata wa fedha, TFF imefunguka na kueleza adhabu hiyo imeshamalizika kwani ilikuwa ni ya miaka mitatu.

TFF imeeleza kuwa kama kutakuwa na mabadiliko mengine juu ya Mtibwa endapo atashinda na uwakilishi wake kimataifa ukaingia dosari, watafanya namna nyingine juu ya mwakilishi.

Mtibwa inakutana na Singida United ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 3-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara katika msimu uliomalizika hivi karibuni. Mechi hiyo itaanza saa 10 kamili kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic