June 2, 2018



Na George Mganga

Kikosi cha Yanga kinafanya mazoezi yake ya mwisho huko Kenya kwa ajili ya kibarua chake cha kwanza cha mchezo wa michuano ya SportPesa Super Cup inayoanza kuwaka moto kesho.

Yanga itaanza mechi yake na Kakamega Home Boys itakayoanza mapema majira ya saa 7 mchana ikiwa ya kwanza kufungua pazia la michuano hiyo.

Kuelekea mechi hiyo taarifa zinaeleza wachezaji wote wa Yanga wako fiti kuelekea mchezo huo ukiwa ni wa safari ya mwanzo kujiandaa kukipiga na Everton huko Goodison Park, England.

Ikumbukwe mshindi wa mashindano hayo atasafirishwa na SportPesa kuelekea England kucheza na Everton ambayo inashiriki Ligi Kuu England.

Morali ya wachezaji wa Yanga inaonekana kuwa vizuri huku nyota wake Amis Tambwe na Thaban Kamusoko wakionekana kuendelea kuimarika kwa ajili ya mechi za michuano hiyo.

Wakati Yanga ikijiandaa kucheza na Kakamega, watani zao wa jadi, Simba wataanza kibarua chao Jumatatu ya wiki ijayo kwa kucheza na Kariobang Charks mida ya saa 9 alasiri.

2 COMMENTS:

  1. Hizi Mechi zitarushwa chanel gani?@salehjembe

    ReplyDelete
  2. Hizi Mechi zitarushwa chanel gani?@salehjembe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic