SIMBA WAUNGANA NA YANGA KUIBOMOA GOR MAHIA, KIUNGO HUYU AHUSISHWA KUTUA MSIMBAZI
Wakati Yanga wakipigania saini ya mshambuliaji hatari wa Gor Mahia FC, Meddie Kagere, Simba nao wameanza kumuwania kiungo nyota na tegemeo wa kikosi hicho, Francis Kahata.
Kahata ameanza kuhusishwa kutua Simba baada ya kung'ara katika mashindano ya SportPesa yaliyomalizika siku kadhaa zililizopita nchini Kenya na Gor Mahia kuweza kuwa mabingwa taji hilo dhidi ya Simba.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 inaelezwa tayari jina lake limeshaanza kupigiwa chapuo na mabosi wa Simba, pengine anaweza akatua hapa nchini siku chache zijazo.
Taarifa zinaeleza kuwa Kocha Msaidizi wa wekundu hao wa Msimbazi, Masoud Djuma, amewasilisha jina la kiungo huyo kwa mabosi wake ili kuweza kumsajili kiungo huyo mahiri kutoka Gor Mahia FC.
Endapo wachezaji hao wawili, Kahata na Kagere wataondoka klabuni hapo, Simba na Yanga watakuwa wameungana kuiboa Gor Mahia.
Kama simba kwelii wanamtaka hakuna jinsi Gormahia watamtema tu. Mimi hizo kelele za Yanga za kutamani kila mchezaji wala si zipi uzito kwani wakati mwengine naona kama kelele zao ni kuichombeza SIMBA ili isiende kubomoa pale jangwani. Wahenga walisema Debe tu kamwe haliachi kelele.
ReplyDeleteHuu ndo utakuwa usajili wa maana kama ikiwezekana coz nimemwangalia alivokuwa unawasumbua mabeki pinzani sio kawaida halafu ana uchu wa mafanikio..
ReplyDelete