June 13, 2018


Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa wa Habari, Haji Manara, umesema kuwa kwa sasa unajipanga kusajili mshambuliaji wa kimataifa kwa ajili ya kuongeza makali ya safu ya ushambuliaji.

Licha ya uwepo wa Emmanuel Okwi na John Bocco ambao walikuwa sehemu ya mchango mkubwa wa Simba katika msimu uliopita, bado mabosi wa timu hiyo wanahitaji mshambuliaji mwingine.

Manara ameeleza kuwa kwa sasa benchi la ufundi linaangalia nani asajiliwe na akishindwa kuweka wazi linatazamia kupata mchezaji kutoka taifa lipi.

Hatua hiyo mara baada ya kikosi hicho kushindwa kufumania nyavu katika michuano ya SportPesa iliyomalizika siku chache zilizopita nchini Kenya ingawa washambuliaji wake tegemeo hawakuwepo.

Usajili huo utakuwa wa tatu kwa Simba baada ya kumalizika kwa ligi ambapo tayari ishaingiza wapya watatu ambao ni Marcel Kaheza, Adam Salamba na Mohamed Rashid.

Aidha endapo kama Simba watafanikiwa kuleta mchezaji huyo watakuwa wanajibu mapigo ya Yanga ambayo ishaanza harakati za kumuwania Meddie Kagere anayeichezea Gor Mahia FC ya Kenya.

2 COMMENTS:

  1. Hivi haiwezekani kuandika habari za Yanga bila kuihusisha simba au habari za simba bial kuihusisha Yanga? Sijaona hapo Yanga wanaingiaje, mnaharibu taaluma.

    ReplyDelete
    Replies
    1. This comment has been removed by the author.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic