June 12, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umezungumzia uvumi wa tetesi zilizoeleza kuwa wapo kwenye mchakato wa kumsajili straika tegemo na hatari wa Gor Mahia FC ya Kenya, Meddie Kagere.

Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Charles Boniface Mkwasa, amefunguka na kusema ni kweli mipango hiyo ipo ila mambo yatakapoiva taarifa rasmi zitatolewa na kila kitu kitawekwa wazi.

Kwa mujibu wa Radio One kupitia kipindi cha Spoti Leo, Mkwasa ameeleza kuwa kwa sasa ni mapema zaidi kuweka kila kitu hadharani na akiomba subira na uvumilivu uwepo ili kila kitu kitakapofikia mwafaka mambo yatawekwa wazi.

"Ni kweli lakini si muda mwafaka wa kuweka kila kitu wazi kwa sasa, naomba subira na uvumilivu viwepo mpaka pale mambo yatakapokuwa tayari tutaweka kila kitu wazi" alisema.

Yanga imeingia katika harakati za kunyaka saini ya mchezaji huyo aliyeng'ara kwenye mashindano ya SportPesa Super kwa kuisaidia Gor Mahia kufika fainali na kuchukua kikombe mbele ya miamba wa soka la Tanzania Simba SC.

Kagere amebakiza mwezi huu wa sita pekee kabla ya ujao mkataba wake kumalizika na Gor Mahia japo yupo huru kuanza mazungumzo na klabu yoyote ile.

Mabingwa hao wa kihistoria katika Ligi Kuu Bara wanapigania saini ya nyota huyo kuja kuimarisha safu ya ushambuliaji baada ya kumalizana na Mbenini, Marcellin Koukpo ambaye inaelezwa ameshaini mkataba wa miaka miwili.

2 COMMENTS:

  1. Yanga inahitajo utulivu na vyanzi vya uhakika vya mapato kwani kwa kikosi ilichonacho sasa kinatakiwa kuimarishwa badala ya kukimbilia wachezaji wanaoneekana hawatakua na maisha marefu kikosini

    ReplyDelete
  2. Ushauri wangu, kama ni kweli mchezaji huyu anataka dau kubwa sh 180 milioni na kama ni kweli umri wake ni miaka 33 basi viongozi wa Yanga wamtake ashuke dau lake angalau sh 80 milioni vinginevyo achaneni naye. pesa anayotaka tutasajili wachezaji 4 watanzania wazuri tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic