SINGIDA UNITED YAUNGANA NA SIMBA NUSU FAINALI SUPER CUP, MANYIKA AWA SHUJAA
Singida United imeungana na Simba kuingia hatua ya nusu fainali ya mashindano ya SportPesa Super Cup kwa ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya AFC Leopards wa njia ya matuta.
Ushindi huo umepatikana na kuiwezesha Singida United kutinga hatua hiyo baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 0-0.
Kipa wa Singida, United, Manyika Junior, ameibuka shujaa wa mchezo huo baada ya kuokoa penati mnamo kipindi cha pili kabla ya dakika 90 hazijamalizika.
Matokeo yanaifanya Singida iungane na Simba huku Yanga na JKU kutoka Tanzania zikiwa tayari zimeshaaga mashindano.
Hongera sana Singida. Beki imecheza vizuri. Manyika ndiye shujaa wa mchezo wote. Lakini washambuliaji kama ilivyokuwa kwa Simba, hawakucheza vizuri. Lazima kupiga mipira golini kwa mpinzani ili uweze kushinda. Simba na Singida huu ugonjwa lazima muutibu haraka huko Kenya. Tunataka magoli sasa mtayapataje kama hampigi mashuti???????
ReplyDeleteAgree
DeleteLakini inasemekana mashabiki wa yanga wanangojea huko ili kuizomea Simba katika nusu fainali. Kwahakika watu wa ajabu
ReplyDeleteUnaweza kupiga mashuki golini, ila golikipa anaweza kuwa mzuri kwa kupangua ama kunyaka mipira. Hivyo yote yanawezekana kama kwa Manyika kupangua na kwa golikipa wa AFC Leopard akafanya hivyo.
ReplyDeleteProtas-Iringa