June 15, 2018


Kufuatia kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwatangaza wachezaji watatu waliobaki katika kinyang’anyiro cha tuzo hiyo ambao ni pamoja na Emmanuel Okwi, John Bocco na Erasto Nyoni ambao wote ni wachezaji wa timu ya mabingwa wa Tanzania Bara 2017/2018, Simba, kamati imetoa ufafanuzi kuhusu tuzo hiyo.

IKwa mujibu wa gazeti la Championi, Said George ambaye ni mjumbe wa kamati ya tuzo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), alisema kuwa kamati haikurupuki katika maamuzi bali wanafuata vigezo vilivyowekwa ili kuhakikisha kwamba wanampata mchezaji anayestahili kupewa tuzo hiyo.

“Kitu cha muhimu ni uwezo wa mchezaji hasa kwa kile ambacho amekifanya kwa timu yake ,uwajibikaji wake ndani ya timu, mafanikio aliyoyakataa katika ligi akiwa na timu yake na kuna vitu vingi sana ambavyo vinatazamwa hasa kwa kuangalia takwimu na hatuangalii timu inayoshiriki hilo sio jambo kubwa sana,” alisema George.

Kwa upande wa ofisa habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema kuwa mchakato umechukua muda mrefu mpaka kufikia hapo na kila hatua walikuwa wanachuja kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa na sio kupitia mapendekezo ya mtu ama timu husika tu.

“Tulianza na kuchagua idadi ya wachezaji 30 hadi ikafika 15 na sasa fainali wamebaki wachezaji watatu hao wote hawachujwi tu kwa kupigiana ana ana anado wanachujwa kwa vigezo,” alisema Ndimbo. 

Okwi, Bocco na Nyoni wamesaidia timu ya Simba kutwaa ubingwa kwa msimu wa mwaka 2017/2018, huku Bocco na Okwi wakiwa wameifungia timu jumla ya mabao 37 kwenye ligi

7 COMMENTS:

  1. Tutaona mengi sana.....hii tifuatifua ya kalio

    ReplyDelete
    Replies
    1. ebu tupe takwimu kwamba atoke nani aingie nani kwenye hao waliotajwa? uje na takwimu za msingi

      Delete
  2. hehehehe yajayo yanafurahisha

    ReplyDelete
  3. Nini daladala...wataenda na baiskeli za miti kwa Manji.Yanga si kwa kuchanganyikiwa hivyo....hadi huruma

    ReplyDelete
  4. Dah wangemuweka hata mchezaji mmoja wa Yanga kama Rostand

    ReplyDelete
  5. Mahaba ya kitu yakizidi kazi lazima iharibike!Sina swali kwa Bocco na Okwi kwa uwezo walionyesha kwa nafasi ya ushambuliaji wameonyesha wao bora kuliko wengine ila Nyoni sitakubali coz nimeona mabeki bora kuliko yeye!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic