Wakati wekundu wa Msimbazi wakijiandaa kwa ajili ya kibarua cha mchezo wa SportPesa Super Cup utakaopigwa kesho katika hatua na nusu fainali dhidi ya Kakamega HomeBoyz FC, mchezaji Mohammed Hussein, amegusia suala la kukosa penati.
Hussein maarufu kwa jina la Tshabalala ameeleza kuwa suala la kucheza penati ni kama bahati nasibu ambayo unaweza ukapata ama ukakosa kutokana na umakini wa mpigaji na anayepigiwa walivyojipanga.
Beki huyo wa kushoto alikosa mkwaju wa penati dhidi ya Kariobang Sharks uliopigwa Juni 4 2018 ambapo ilpaa juu ya lango, ingawa haikuleta athari kutokana na Simba kuweza kushinda kwa jumla ya penati 3-2.
Penati siyo nzuri, ni kama bahati nasibu. Tulikuwa na mpango wa kushinda ndani ya dakika tukashindwa dhidi ya Sharks lakini tutarejea tukiwa tofauti ili tuweze kushinda," alisema Mohamed Zimbwe 'Tshabalala'.
Mabli na suala la penati, kuelekea mechi ya kesho, Tshabalala ameahidi kikosi chao kuja kivingine ili waweze kupata ushindi na hatimaye kutinga fainali na ikiwezekana kuchukua ubingwa.
Simba inashuka dimbani Afraha Stadium kesho Alhamis majira ya saa 9 alasiri kukipiga na Kakamega waliondoa Yanga mashindano, ambapo mshindi wa mechi hiyo atatinga hatua ya fainali.
Maelwzo ya kujifurahisha. Tshabalala anakosa penalti kila siku. Tsabalala anasema walipanga kushinda ndani ya dakika 90 inawezekanaje wakati wamepiga shuti moja tu golini kwa wapinzani? Ukweli timu haikucheza vizuri. Pigeni mashuti kama walivyofanya wapinzani au jana AFC Leopards wamepiga mashuti safi golini kwa Singida. Timu yetu ya Simba haipigi mashuti golini kwa wapoinzani ajabu kila mpira wanarudisha nyuma eti ndivyo mwalimu amewafundisha. Binafsi inaniuma sana.
ReplyDelete