Beki Mohamed Zimbwe maarufu kama Tshabalala alikataa kupiga mkwaju wa penalti kabla ya kulazimishwa kufanya hivyo na kocha wake, Pierre Lechantre.
Zimbwe alikosa penalti wakati Simba ikiivuka hadi nusu fainali ya Kombe la SportSuper Cup. Hiyo ilikuwa ni mara yake ya tatu akikosa.
Moja ya vyanzi vilieleza kwamba Zimbwe maarufu alimuomba kocha wake asipige, lakini kwa kuwa siku hiyo alikuwa nahodha alimlazimisha apige.
"Kocha alilazimisha alitaka akapige, alipomuomba asipiga alimuambia lazima aheshimu uwezo wake," kilieleza chanzo.
Taarifa nyingine zilileza kwamba Pamoja na Tshabalala, Paul Bukaba yake aliomba asipige penalti lakini kocha huyo raia wa Ufaransa alisisitiza lazima apige, naye alikosa.
Kikosi cha Simba kimeapa kubadilika katika mechi yake ijayo ya michuano ya Kombe la SportPesa Super Cup.
Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amesema wanaamini hawakucheza katika mechi yao iliyopita ya michuano hiyo mjini Nakuru.
Mmecheza VIBAYA nashangaa baadhi ya viongozi wetu hawapendi kujikosoa sasa unataka tusifie kitu cha uongo? Huo uongozi gani? Hatukanwi mtu ila tunaelezana ili tujisahihishe. Dakika 90 tumepiga shuti moja tu golini kwa wapinzani wetu. Mipira yote tunarudisha nyuma nakuishia katikati, leo utasemaje tulipanga tushinde? Lazima forward line ipenetrate ngome za wapinzani wasiogope na kurudisha mipira nyuma bila sababu. Tunataka Simba ifunge magoli.
ReplyDeleteNi sahihi kabisa. Mpira ni magoli. Hakuna faida ya kucheza mpira na kupasiana nyuma. Kuna wafungaji wazuri Simba kama Marcel na Mohamed Rashid, watumieni vizuri.
Delete