June 11, 2018


Na George Mganga

Tuzo za Simba Mo Awards zinafanyika leo katika ukumbi wa Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo zitakuwa maalum kwa watu wa klabu hiyo waliofanikisha Simba kufanya vizuri kwa msimu wa 2017/18.

Wanachama, viongozi, mashabiki na matawi ya klabu hiyo yatahusishwa katika ugawajwi wa tuzo hizo zitazofanyika leo kuanzia saa 12 kamili jioni.

Kwa mujibu wa mwanzilishi ambaye ni mwekezaji mpya wa klabu hiyo, Mohammed Dewji 'Mo', amesema lengo mahususi la kuanzisha tuzo hizo ni kutambua mchango wa waliofanikisha Simba kufikia hapo ilipo.

Baadhi ya vipengele ambavyo vitakuwepo katika ugawajwi wa tuzo hizo ni mchezaji bora wa mwaka, kiungo, mshambuliaji, shabiki na zinginezo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic