June 19, 2018



Yanga wameamua kufanya usajili wao kwa uficho kwa hofu ya kupokonywa tonge mdomoni na wapinzani wao ambao wanaonekana kuwa wako vizuri kifedha.


Mmoja wa wajumbe wa kamati maalum ya Yanga, ameaimbia SALEHJEMBE kwamba wamekuwa wakifanya mambo yao kimya kutokana na hofu ya kuwaingiza inaowataka katika vita ya kuwaniwa na Simba au Azam FC.

"Sisi hatuko vizuri sana kifedha ndugu yangu, tunachofanya ni kutafuta wachezaji kwa ushauri wa wataalamu na hasa makocha na kuangalia mapendekezo sahihi.

"Baada ya hapo, usajili wetu unakuwa wa kimyakimya sana. Unajua wenzetu wakisikia mchezaji anatakiwa Yanga hata kama hawamtaki, basi wanamsajili tu, sijui ni kukomoana," alifafanua.

Hadi sasa Yanga bado haijafanya usajili unaoeleweka na imekuwa ikielezwa suala la ukata wa kifedha limekuwa tatizo kuu linalowatatiza.


8 COMMENTS:

  1. Kwa hiyo taarifa za Yanga kumsajili mbenini ambazo zilitolewa na blog hii zilikuwa ni za uongo hadi leo hii utuambie kuwa Yanga haijafanya usajili wowote wa maana?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tatizo la blog hii inapost habari nyingi za kuokoteza mtaani kiasi cha kuwafanya hata waandishi wake kupoteza kumbukumbu.Si ajabu blog hii kutoa taatifa moja asubuhi,jioni ikakanushwa na taarifa nyingine.

      Delete
  2. Sio lazima kutoa habari za Yanga na Simba, hii habari unaiandika ni mara ya tatu au nne. Tatizo lenu mnaandika udaku mno kiasi kwamba mnapoteza hadi kumbukumbu.

    ReplyDelete
  3. Uongo mwingine wa waziwazi. Kiongozi gani wa Yanga uliyemkariri akisema maneno ya kusajili kimyakimya kwakuwa hawana fedha? Mnawadanganyia watu na kuweka maneno yenu midomoni mwao. Huo sio uandishi acheni kudhalalishana.

    ReplyDelete
  4. Ni blog inayotoa taarifa negative za Yanga mara nyingi ni blog inayompa coverage kubwa mzee Akilimali kuliko viongozi halali wa Yanga..unaweza kutambua nia yao ya wanayoyafanya.

    ReplyDelete
  5. Kwani ukiwa huna hela ndo unasajiri kimya? we muandishi gani. hivi nyie kila siku habari Negative kwa Yanga,nani anawatuma au ndo uwezowenu. tz tuna timu nyingi je yanga ndio inayosajiri pekee. Acha ujinga wako,we ukiamka ni Yanga.

    ReplyDelete
  6. Kama hamna uthibitisho wa habari za usajili kwanini uandike? Miiko ya uandisbi haifuatwi kabisa.

    ReplyDelete
  7. Reply

    Al LecJune 19, 2018 at 4:49 PM
    Kama hamna uthibitisho wa habari za usajili kwanini uandike? Miiko ya uandishi haifuatwi kabisa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic