June 15, 2018
Timu ya Arab Contractor ya Misri ni kati ya zile ambazo zinaonyesha kuwania saini ya mshambuliaji Obrey Chirwa.


Mmoja wa maofisa wa Arab Contractor aitwaje Azeem Said amesema kwamba wanahitaji saini ya Chirwa baada ya kuangalia ushiriki wake wa kimataifa.

“Tunamhitaji, kawaida timu inaweza kuzungumza na wakala wake halafu klabu. Tayari tumefanya mawasiliano ingawa tumeambiwa anaweza kwenda nchini nyingi.

“Bado tunaendelea kufuatilia ili kupata uhakika. Tunahitaji mshambuliaji wa aina hiyo na kocha amesisitiza,” alisema.
Alipoulizwa mmoja wa viongozi wa Yanga, alisema wao wamelisikia suala hilo juujuu, lakini bado wanaendelea kusubiri.

“Ila mimi si msemaji wa klabu, hata hivyo tumelisikia hilo lakini ni suala la kusubiri,” alisema.

Chirwa alionekana kuwa na kasi nzuri ingawa mwishoni mwa Ligi Kuu Bara, alionekana kupoteza kasi yake.

1 COMMENTS:

  1. Alipoteza kasi kwakuwa walikuwa na mgomo baridi kutokana na kutokulipwa kwa muda wa miezi mitatu

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV