June 2, 2018


Huku taarifa za chini kwa chini zikielezwa kuwa Simba inamuwinda kwa udi na uvumba mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa, imeelezwa waarabu wameingilia kati mpango huo.

Klabu ya Ismailia ya Misri imeingilia rada za Simba kuhusiana na usajili wa Mzambia huyo ambapo taarifa zinasema imeanza mazungumzo ya kuweza kumnyaka mchezaji huyo tegemeo kwa Yanga.

Chirwa ameshindwa kujumuika na kikosi cha Yanga kuelekea Kenya kwa ajili ya michuano ya SportPesa Super Cup inayoanza kesho.

Waarabu hao wameanza kuifanyia umafia Simba ambapo inaelezwa wameandaa dau nono zaidi ya Simba hivyo kuweka ugumu wa kujiunga na wekundu hao wa Msimbazi ambao wanatajwa kupigania saini yake hivi sasa.

Mzambia huyo amekuwa akiwindwa na Simba ingawa mwenyewe amekuwa akieleza kuwa anatamani kucheza soka la kimataifa hivyo kuna hatihati kama anaweza akasalia Tanzania msimu ujao.

Uwezekano mkubwa wa Chirwa kuondoka Yanga unawezekana kutokana na mchezaji huyo kugoma mara kadhaa kusafiri na timu pale inapotoka kwenda nje ya nchi kushiriki mashindano ya Kimataifa, ikielezwa kuwa anaidai stahiki zake ikiwemo mishahara.

3 COMMENTS:

  1. I think if Obrey Chirwa go on and playing for Simba next season will be a right decision for several reasons. SIMBA is the Tanzanian champion so will have the opportunity to compete in an international level next year. Chirwa has already had familiar with the Tanzania environment and if it is true that Simba want to recruit him for next season that will make all the sense for him to be a part close to his own country. Last and the most important thing Simba is not Yanga where he had a hard time getting his salary being paid but at SIMBA it is total different situation where he will get paid on time and even better payment. I remember when first Chirwa come to Tanzania he had a real tough time at Yanga to prove that he was a player worth for the money but then if he want to go on and start a new life in a Arab country it is up to himself except he has to be ready for even much more hard time than he encountered in Tanzania.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unambembeleza kwa kimombo, hahahaha muhakikishie malipo yake moja kwa moja toka kwenye akaunti ya klabu.

      Unadhani yy ni mjinga utajiri Wa vilabu unaotegemea mifuko ya watu.

      Kwa ushabiki mpeleke PANYA FC kwa mstakabali Wa maisha yake ya soka na utajiri aende Misri.

      Umeeleza sawa mazingira ya soka la Tanzania anayajua uvumilivu aliopata Yanga hawezi upata Simba.

      MF MAVUGO, LUIZIO wanajuuuuuuuuta.

      Delete
  2. What he expects to earn in foreig countries can easily earn here from team leader. The player is already aware of Tanzania culture and its people, but nothing of where he intends to go.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic