Nyota wa Atletico de Madrid na timu ya Taifa ya Ufaransa, Antoine Griezmann, amesema kuwa hatima ya yeye na klabu yake itajulikana mapema kabla ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu kuanza.
Griezmann amekuwa akihusishwa na timu kadhaa zinazotaka kumsajili barani Ulaya huku FC. Barcelona wakipewa nafasi kubwa ya kumpata.
Nyota huyo ameeleza kuwa hatima ya kuendelea kusalia Atletico ama kuondoka itajulikana ikiwa ni siku chache zimesalia kabla ya mashindano ya Kombe la Dunia hayajaanza.
Mbali na Barcelona, Manchester United nayo ilishaingia kwenye rada za kumsajili nyota huyo aliye katika fomu hivi sasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment