WAKATI BOCCO AKITANGAZWA KUWA BORA LIGI KUU, MCHEZAJI HUYU BONGO ALITABIRI HIVI
Na George Mganga
Wakati tuzo za Ligi Kuu Bara zikifanyika jana katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, mchezaji na beki wa Stand United, Ally Ally alikuwa tayari ameshafanya utabiri wake.
Yakiwa yamesalia masaa machache kabla ya kuanza kwa tuzo hizo, Ally alimtabiria John Boco kutwaa tuzo na kuwanyima nafasi Emmanuel Okwi na Erasto Nyoni.
Ally alimpa nafasi Bocco ambaye alifanikiwa kutwaa kutokana na kueleza kuwa mchango wake ulikuwa mkubwa ndani ya Simba kwa msimu uliomalizika.
Mchezaji huyo aliongeza kuwa si kwamba Okwi na Nyoni hawakuwa vizuri, bali kwake ameona kuwa Bocco ndiye aliyeiweka Simba katika mhimili mzuri na akiisaidia kuelekea harakati za kuchukua ubingwa ambao ilikuwa haijautwaa kwa muda mrefu.
Bocco ambaye ni Nahodha Mkuu wa Simba, alijitwalia kitita cha shilingi za kitanzania milioni 13 kama mchezaji bora wa msimu wakati Emmanuel Okwi naye akibeba milioni 3 za tuzo ya Ufungaji bora kwa kuwa na mabao 17.
Boko yupo vizuri ana umbo la kuwa centerfoward asilia ila anatakiwa kuzitafuta filamu za hayati Majidi Musisi yule Uganda si kwa mpira tu bali physical structure and strength. Boko wa msimu uliopita na huu wa ubingwa kwa Simba yupo tofauti kwani ameimprove hata kinguvu lakini bado ananafasi ya kuujaza au kuujenga mwili wake kuwa mgumu zaidi na kuwa tishio zaidi. Boko anakimo kizuri ambacho kinampa nafasi ya kujaza nyama zaidi mwili wake misili ya akina Drogba na hakuna kisichowezekana ni mazoezi tu na good diet.
ReplyDelete