June 13, 2018


Waziri wa Maliasili na Utalii nchini, Hamis Kigwangalla ameutaka uongozi wa Simba kufanya mapema ujenzi wa Uwanja uliopo Bunju ili kuendana na hadhi ya klabu hiyo iliyopo hivi sasa.

Ikumbukwe ujenzi wa Uwanja huo ulisimama baada ya nyasi kukwama bandarini kutokana na kushindwa kulipiwa kodi ikiwa na pamoja na sakata la viongozi wa klabu, Rais Evans Aveva na Makamu wake, Nyange Kaburu kuwa na kesi mahakamani.

Kingwangalla ameeleza kuwa hadhi ya Simba ilipofikia hivi sasa klabu inapaswa kuwa na Uwanja wake huku akisema ni wakati mwafaka wa kuanza kuujenga ule wa Bunju ili walau kuelekea msimu ujao timu ianze kuutumia kwa mazoezi.

Waziri huyo aliyasema hayo mapema mara baada ya kumalizika kwa ugawajwi wa tuzo za Mo zilizofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency Hotel, Dar es Salaam.

Tayari Simba ilishabadilisha mfumo wa uendeshwaji kutoka ule wa kuendeshwa na ada za wanachama mpaka uwekezwaji ambapo Bilionea kijana, Mohamed Dewji amekuwa mwekezaji mkuu ndani ya klabu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic