June 13, 2018


Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika klabu ya Simba, Haji Manara, amesema kuwa kutokana na mabadiliko ambayo Simba imeyafanya, kila mchezaji anatamani kusajiliwa nayo.

Manara amejigamba kwa kusema kuwa katika soka la Tanzania hivi sasa Simba ndiyo timu pekee inayolipa mishahara vizuri na vilevile mchezaji yoyote anatamani kujiunga Simba.

Kiongozi huyo amefunguka wakati akizungumzia mipango yao ya usajili ndani ya klabu ambapo benchi la ufundi limeanza mchakato wa kupata mshambuliaji wa kimataifa.

Tayari Simba wameshaanza kumuwinda mshambuliaji huyo ambaye hajaelezwa atakuwa anatokea nchi ipi huku ukieleza inabidi tusubiri mpaka wakati mwafaka utakapofika.

Wakati Manara akieleza hayo, kikosi cha Simba kimepewa mapumziko ya wiki moja na baada ya kumalizika kitaingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya KAGAME inayoanza Juni 28 2018 jijini Dar es Salaam.

11 COMMENTS:

  1. Mimi bado nipo kwenye mashindano ya sports pesa ambayo Simba alionekana misili ya Sungura badala ya kuwinda akawa anawinda yeye. Labda kama kuna kiongozi watanzania wanatakiwa kuwa makini sana na kumsikiliza analozungumza basi ni muheshimiwa raisi JOHN Magufuli kwani huzungumza kutokana na uhalisia wa mambo bila kupindisha ukweli. Alipowakabidhi Kombe simba aliwaambiwa wazi kwamba hakufurahishwa na kiwango chao walichomuonesha siku ile. Na kama vile haitoshi akatilia mkazo kuhusiana na mashindano ya kimataifa timu za Tanzania zianze kushinda kwani tumefungwa vya kutosha lakini inaonekana kana kwamba kauli ya Muheshimiwa rais Simba waliachana nao pale pale uwanja wa taifa huku wakijiandaa na safari ya nakuru yakwenda kuizika kabisa kauli mbiu ya Muheshimiwa rais.

    ReplyDelete
  2. Hakuna timu isiyofungwa.Pamoja na kuwa nä wachezaji wazuri .Simba wamefanya juhudi sana nä kumaliza wa 2.Na kuwa timu ya Tanzania iliyofanya vizuri kuliko zote tena bila kuwa na wachezaji wake wote wa timu ya kwanza. Simba endelezeni bidii ili mfanye vizuri zaidi.Msisikilize kelele za chura.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona hata singida na Yanga walikuwa na wachezaji wa kikosi cha pili pia. Yanga imecheza mwaka mzm ns kikosi cha pili. sema ukweli timu zetu hazikusajili timu zilizokamilika.

      Delete
  3. Mh Rais hakueleweka vizuri, baada ya kasema tumechoka kufungwa Kuna timu sasa Ndio hawataki tenahata kucheza
    Sasa sijui watajificha mpaka Lini

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  5. Mimi ninaamini ingekuwa wachezaji nyota wa simba kikosi kamili kikijumlisha akina Boko, Okwi, Kotei, Murshidi na Asante Kwasi chini ya uongozi wa Masud Djuma, Mambo yangekuwa mengine. Ikumbukwe kuwa Kikosi cha Kenya kilisheheni nyite wake kamili na Simba kutumia wengi kikosi cha pili nila ya kuwatumia wale waliofikisha kila mmoja mabao 20 na 15 na juu ya hiyo kumaliza wapili

    ReplyDelete
  6. Kwa maoni hayo basi hatuna sababu ya kuwacheka Yanga maana nao ilibidi mechi zao za mwisho watumie kikosi cha pili baada ya wachezaji wao wengi kusemekana kugoma kimtindo

    ReplyDelete
    Replies
    1. wakati yanga wanalalamika kukosa wachezaji wa kikosi cha kwanza wao walikebehi na kusema wao wana kikosi kipana wakati ukweli kila mechi waliokuwa wanacheza ni walewale.

      Delete
  7. Tofauti ni kufungwa mechi 7 mfululizo. Mpaka hata kushiriki hawataki. Vipigo imezidi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic