Inaelezwa kuwa straika hatari wa Gor Mahia FC, Meddie Kagere anahitaji kitita cha milioni 180 ili aweze kutua Yanga tayari kuanza kazi rasmi.
Kagere ambaye amebakiza mwezi mmoja pekee kumaliza mkataba wake na Gor Mahia anawindwa na Yanga ili kuchukua nafasi ya Donald Ngoma aliyeondoka klabuni hapo kuelekea Azam FC.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka Kenya zinaeleza kuwa Kagere ameweka dau la milioni 180 na akiomba awe analipwa mshahara wa milioni 11 kwa mwezi ili aweze kuja kukipiga na mabingwa hao mara 27 wa Ligi Kuu Bara.
Mbali na Yanga, klabu ya Singida United nayo imeanza kupiga chapuo kwa mchezaji huo ambaye amepewa asilimia kubwa kujiunga na Yanga.
Kagere amejizoea umaarufu mkubwa hapa nchini baada ya kuifunga Simba na kufanya vizuri katika michuano ya SportPesa Super mjini Nakuru, Kenya kwa kuisadia Gor Mahia kubeba ubingwa wa mashindano hayo.
Yanga anawafaa sana akishirikiana na anko ngasa
ReplyDeleteHilo jembe la kazi karibu kwa mabingwa mara 27
ReplyDelete