June 7, 2018


Taarifa zinasema kuwa viongozi wa Yanga wamekanusha habari zinazoeleza kuwa wameanza kuufanyia ukarabati Uwanja wa Kaunda ili kujitengenezea mazingira ya kupata kura kuelekea uchaguzi mkuu.

Yanga inatarajia kufanya uchaguzi hivi karibuni baada ya kupewa msisitizo na Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kutokana na kukaa kwa muda mrefu bila ya kuwa na Mwenyekiti wa klabu.

Wakati vuguvugu la uchaguzi likianza kushika kasi kwa sasa, Uwanja wa Kaunda uliopo katika makao ya klabu hiyo umeanza kufanyiwa ukarabati ili uweze kutumika kwa ajili ya mazoezi ya timu.

Wakati ukarabati huo ukiendelea uongozi wa Yanga umesema wanafanya hivyo si kwa kujitengenezea nafasi za kupewa kura bali ni kwa maslahi mapana ya klabu.

Tayari kifusi kimeshawekwa kwenye Uwanja huo ambao ulikuwa unatuamisha maji kwa wingi kiasi cha kwamba kupelekea maji mengi kutuama lakini kwa sasa kumekuwa na mabadiliko.

Yanga inaenda kufanya uchaguzi huo ili kujaza nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wake, Yusuph Manji aliyejiuzulu akiomba apumzike.

Mbali na Mwenyekiti, Yanga pia itakuwa inachagua Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ikiwemo wale waliojizulu ambapo mmoja wao ni Salum Mkemi.

2 COMMENTS:

  1. Kwani ni kosa? Binadamu hatuna jema. Chapeni kazi Mkwasa na wenzio nyinyi ni viongozi mliopo madarakani man wajibu wa kutekeleza miradi ya klabu,kosa lipo wapi??

    ReplyDelete
  2. hizo habari zilienezwa wapi. toa taarifa iliyokamilika. kazi ya kiongozi ni kufanya maendeleo sehemu alipo.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV