June 2, 2018


Wakati vuguvugu la usajili Bongo likiwa linaendelea, tetesi zinaeleza kuwa Yanga imemalizana na Mshambuliaji Mbenin, Marcellin Koukpo, aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Buffles du Burgou nchini kwao.

Yanga ambayo usajili wake unaonekana kuwa wa kimyakimya haijaweza kuweka wazi kuhusiana na kumyaka mshambuliaji huyo ambaye inaelezwa amekuja kuchukua nafasi ya Donald Ngoma aliyetimkia Azam FC.

Taarifa zinaeleza kuwa Koukpo amesaini mkataba wa miaka miwili kuwatumia mabingwa hao wa historia katika Ligi Kuu Bara kwa kuutwaa mara 27.

Imeelezwa pia mchezaji huyo ataungana na kikosi cha Yanga nchini Kenya, tayari kwa michuano ya SportPesa Super Cup inayoanza kesho.


6 COMMENTS:

  1. Moja kati ya kitu ambacho Yanga inatakiwa kuepukana nacho katika kipindi hiki cha majaribu ni kutaka kushindana na Simba hasa katika masuala ya usajili. Hata msimu uliopita watu hawazungumzi kwa uwazi lakini kitendo cha Yanga kujitutumua kuhakikisha wanaendelea kuwabakisha akina Ngoma ndiko kulikowaingiza mkenge. Wakati SIMBA ilipokuwa katika hali ngumu ya kiuchumi viongozi wao waliekeza kwenye hali nzuri zaidi ya kiakili kwa kufanya zoezi la kutafuta vijana wa kitanzania angalau wenye mapenzi na Simba kwa kuwaelea na kuitumukia klabu yao na kama si figisu la uongozi wa TFF uliopita basi SIMBA bingwa hata msimu uliopita. Wakati mwengine sisi watanzania ni wanafiki sana au niseme sio wakati mwengine bali kiuhalisia sisi watanzania ni wanafiki hadi kichefu chefu. Utasikia kelele za kiunafiki kutoka kwa wadau wanaojifanya watu wa mpira kwamba bila soka la vijana hatuwezi kusonga mbele kimpira, ni kweli lakini SIMBA walianzisha mradi huo kwa dhati kabisa wa kulea vijana wengi lakini cha ajabu badala ya SIMBA kupewa sapoti walipigwa vita kila kona,wakati huo walisema,Ooh SIMBA haiwezi kuwa bingwa kwa sababu imekumbatia vijana inapaswa kuajiri watu wazima wa kazi,jamani subira huvuta kheri na si hivyo tu haohao wachezaji wake vijana waliokuwa wakibezwa wakaanza kusainishwa kwenda vilabu vyengine kinyemela kwa baraka za TTF. Unajua Binaadamu sio malaika na wanasema ukienda nchi karibu watu wake wote wanatumia jicho moja kuona na wewe kwa busara unatakiwa kufumba jicho lako moja ili ukubalike kwenye jamii yao na kama utaleta ubishi ya kujifanya wewe unaona sana basi si ajabu wakayatoboa macho yako yote usione kabisa. Simba naweza kusema waliachana na masuala ya kuwatumia vijana na vijana wake wengi wametapakaa klabu mbali nchini lakini sio jambo la kufurahia hata kidogo kwa maendeleo ya soka nchini. Spain sio Zamani sana walikuwa sio nchi ya kuwaumiza vichwa vigogo wa soka Duniani kama Brazil, Argentina, Germany,Italy au hata England. Lakini la Masia ya Barcelona imekuja kubadilisha kila kitu katika mpira wa Spain na nnaimani kama SIMBA wangepewa ushirikiano wa kutosha basi leo Tanzania isingekuwa na tatizo la first eleven ya maana kwenye timu yetu ya taifa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mmmmmmmh kwa point ipi inayokufanya useme simba angekuwa bingwa.....umeongea point but punguza ushabikiiiiiiiiii....unaposema simba walifanya vizuri mwaka gani???? mbona hawakushiriki kimataifa???? acha unazi bhana

      Delete
    2. Ukweli japo wakati mwingine unauma lkn ukweli utabaki ukweli. Nakubaliana nawe Simba imejitahidi sana kukuza vijana na ukiangalia timu karibu asilimia 80% ya wachezaji waliocheza VPL hakukosekana mchezaji aliyepata kuchezea Simba na wengi wao wakiwa wametoka Simba B.Lkn kwa kuwa sasa mpira ni ajira na pesa inabidi izungumze.
      Yanga inabidi wawe makini na mawakala wanaowatafutia wachezaji toka nje maana isije ikaishia kuleta wachezaji ambao hata kwenye ndondo wanapatikana

      Delete
  2. Tatizo usajili wa staili hii mnaweza kuingizwa mkenge. Tulikuwa na mchezaji mmoja wa kigeni hapa nani vile? YAW ?au mmeshasahau?

    ReplyDelete
  3. Ninachofahamu habari hizi zinetungwa tu na huyu jamaa siku hizi haaminiki kwa habari. Hana ukweli wowote

    ReplyDelete
  4. Hapo ndio nabaki kuwashangaa hawa viongozi wa Yanga maana wametuambia uchumi wa kipesa Yanga haiko vizuri na lundo la wachezaji wanadai mishahara na wengine pesa zao hajamaliziwa za usajili.Lkn hapo hapo wanasajili mchezaji toka nje. Sasa tuwaeleweje viongozi wetu wa Yanga?..kwa nini kwanza msimalizane na wachezaji ambao wameshavuja jasho lao?...hii ni biashara ya utapeli tu yaani ni sawa na ya Ngoma. Nahisi kuna harufu ya utapeli.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic