JERRY MURO KURIPUA BOMU JINGINE KWENDA UONGOZI WA YANGA LEO
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, jJerry Muro, amesema leo sikukuu ya EID anaripua bomu jingine tena kuhusiana na namna mwenendo wa klabu hiyo unavyoenda hivi sasa.
Muro amekuwa akiwashutumu viongozi wa Yanga kwa kitendo chao cha kumuondoa aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mholanzi, Hans nav der Plujim, akieleza ndiyo sababu kubwa ya timu kuanza kupata matokeo mabovu.
Muro ambaye aliwahi kuwa kwenye kitengo hicho wakati Mfanyabiashara, Bilionea, Yusuph Manji akiwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, amesema leo atatoa waraka mwingine kuhusiana aina ya watu ambao wanatakiwa kuiongoza klabu.
Kupitia waraka wake alioutoa jana na kuwekwa kwenye blog hii, Muro alieleza Yanga ya sasa inahitaji mtu atakayeweza kuwekeza na si tajiri ambaye atakuwa anatoa tu fedha zake.
Waraka huo ulikuwa na mengi aliyoyaeleza na mojawapo ni kuhusu uwekezaji akiwataka viongozi wafanye mchakato wa kukaribisha mwekezaji ili klabu iweze kuingia katika mfumo mpya kiuendeshwaji kama ambavyo Simba wameanza hivi sasa.
Mchumia tumbo tu huyo hana lolote! Anahangaika kutafuta fadhira za makonda.
ReplyDeleteAngeyasema yote hayo kabla hajasimamishwa kazi tungemuona mpigania haki bt Leo analopoka kwa kuwa kafutwa kazi mwambieni aache kuwakatisha tamaa viongoz wamepambana ktk kipnd kigumu wala hawakuikimbia club
ReplyDelete