July 23, 2018




Baada ya usiku wa kuamkia jana Jumapili Simba kukwea pipa kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kambi yake, nahodha wa kikosi hicho ambao ni mabingwa wa ligi kuu msimu uliopita, John Bocco ameweka wazi faida ya kambi hiyo.

Bocco alikuwa sehemu ya wachezaji ambao waliondoka na kikosi hicho cha Simba chini ya kocha Patrick Aussems, raia wa Ubelgiji kuelekea Uturuki walipokwenda kuweka kambi ya wiki mbili kabla ya kurudi nchini Agosti 5, mwaka huu, kwa ajili ya Simba Day itakayofanyika, Agosti 8.

Mshambuliaji huyo ambaye ameibuka Mchezaji Bora wa timu yake na Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2018/19 amesema kwake kama nahodha anafurahi kuona wanapata sehemu ya utulivu ya kuweka kambi ambayo itawajenga kisaikolojia kwa ajili ya kupambania kutwaa ubingwa wa ligi kwa msimu ujao.

“Msimu uliopita tulikuwa hapahapa Afrika na tukaenda Afrika Kusini kwa ajili ya kambi ya pre season, lakini kwa msimu huu tunaenda Ulaya katika nchi ya Uturuki, kwangu ni jambo zuri kwa sababu tunaenda kupata kitu kipya kabisa tofauti na kama tungebaki hapa nyumbani.

“Ninaamini hii itakuwa mwanzo mzuri kwetu kwa ajili ya kutetea ubingwa, unajua tukiwa huko tutapata nafasi zaidi ya kufikiria mazoezi na kuwa fiti zaidi kwa sababu tuko kwenye mazingira salama ambayo yanakufanya kama mchezaji kuwaza mazoezi pekee,  hivyo hilo litakuwa jambo zuri kwetu kuelekea mapambano ya msimu ujao,” alisema Bocco.

SOURCE: CHAMPIONI



2 COMMENTS:

  1. hatari sana...kwa simba hili hapa kagele pale okwi huku bocco lazima serikali iingilie kati...na hivi tushaona wanapigika 4G hovyo hovyo...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli kabisa hapa inabidi serikali iinglie kati kuinusuru mayebo ambao tayari wanapata taabu sana. Wakiifikiria tu simba magoti yanaregea

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic