July 23, 2018


Na George Mganga

Rasmi Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, ametangaza kujiuzulu wadhifa wake katika klabu hiyo.

Sanga amejiuzulu wadhifa huo kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri baina yake na viongozi wenzake ndani ya klabu hiyo ikiwemo wale wa Kamati ya Utendaji kueleza hana ushirikiano mzuri.

Kiongozi huyo aliyekuwa akikaimu nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, alikuwa akitupiwa lawama na viongozi wa Kamati ya Utendaji akiwemo Khalfan Hamis ambaye amejiuzulu juzi akidai Sanga amekuwa si mweledi wa mambo.

Mbali na kukosa maelewano, Sanga ameeleza kuwa kuna CLIP ameiona mitandaoni inayohamasisha watu kumvamia kwa mapanga ni moja ya sababu zilizopelekea kufanya uamuzi wa kuachia ngazi.

Aidha,wiki kadhaa zilizopita Mjumbe mwingine kutoka kamati hiyo, Salum Mkemi naye aling'atuka kuendelea na wadhifa huo ndani ya Yanga na akisalia kuwa mwanachama pekee kutokana na kutokuwa na kukosa maelewano mazuri baina yake na wanachama wa klabu.

Ukiachana na Sanga, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Charles Boniface Mkwasa naye amethibitisha rasmi kuachia ngazi leo kutokana na kusumbuliwa na masuala ya kiafya.

Mbali na Mkwasa, tetesi zinaeleza kuwa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, naye anatajwa kuanchia ngazi ingawa juzi aliibuka na kukanusha uwepo wa taarifa hizo ambazo zimesambaa kwa kasi mitandaoni.8 COMMENTS:

 1. Replies
  1. Leo yamekuwa haya ama kweli binadamu hachelewi kusahau

   Delete
 2. Hapa ndipo tunasema tubadilishe Mifumo ya uendeshaji wa vilabu vyetu kwa kuondoa suala la vilabu kuwa vya wanachama tunahitaji kuwa na watu wanao kuwa na HISA. Wanachama wanapiga kelele wee, lakini hwana mchango wowote kutoa 1,000/= ni shida leo wataka usajili mzuri, timu ishinde haiwezekani wanayanga! Tutaendelea kurejea kule kule

  ReplyDelete
  Replies
  1. Ndio wengine wao leo wanajisahaulisha kuwa wachezaji wa bei mbaya ndio waliinyanyua Yanga.

   Delete
 3. Waende Tu yanga waliikuta na itaendelea kuwepo!

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV