Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake, Haji Manara, amefunguka kwa kueleza mambo kadhaa ya kupoteza KAGAME dhidi ya Azam.
Simba walishindwa kutwaa taji hilo kwa mara ya 7 kwa kipigo cha mabao 2-1 mbele ya Azam katika Uwanja wa Taifa jana.
Kufuatia kipigo hicho, Manara amesema lengo la kutumia kikosi mbadala na kile kilichocheza ligi kuu msimu uliopita lilikuwa na maana yake katika timu.
"Kabla ya Kagame Cup tuliitisha Press Conference na kuwaeleza watanzania kikosi Kitakachotumika na kwanini baadhi ya Wachezaji hawatotumika."
" Tuliwaeleza pia faida ya Kuwatumia wachezaji wengine haswa wale wapya na wale wengine ambao hawakupata muda wa kucheza msimu Uliopita . sote tunakumbuka zile Lawama za baadhi ya wachezaji Kutocheza Leo tumeona faida yake."
" Yupo mtu atataka kazimoto aachwe? Au Rashidi Juma asiwemo katika timu? Kuna faida kubwa kwa Uamuzi Uliofanywa na benchi la ufundi ama hakika Utalipa. "
" Najua baadhi yenu ni Vigumu kuelewa ila kupanga ni kuchagua na chaguo lao ndio Uamuzi sahihi ambao muda si mrefu mtapongeza" amesema.
Manara uko sahihi unalosema lkn kuna wabishi wa kuzaliwa nao hawatakuelewa.Kazimoto bado ni mchezaji wa kiwango cha juu...umri umeenda?...Ronaldo ana umri gani?
ReplyDeleteKwangu mie uko sahihi kabisa.
ReplyDeleteHATA MIMI UKU SAHIHI KABISA MANARA.
ReplyDeleteNimekuelewa kabisa manara
ReplyDeleteNisawa sasa hao wengine wangecheza lini lengo letu limetimia sasa tunavikosi viwili vilivyokamili kwa mapambano
ReplyDeleteUnapoamua kumwacha mchezaji unamtafutia sababu za wazi, kila mtu kaona Kuna wachezaji wanamajina makubwa Ila hawatufai wameshuka viwango. Kila mtu kaona.mlifanya vizuri
ReplyDelete