July 14, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umeipongeza Azam FC kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya CECAFA KAGAME kwa mara pili mfululizo.

Pongezi hizo zimekuja kufuatia Azam kuwapa kipigo watani zake Yanga, Simba SC, jana kwenye mchezo wa fainali iliyopigwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo Azam walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 yakifungwa na Shaban Idd pamoja na Aggrey Morris, huku la Simba likipachikwa kimiani na Meddie Kagere.

Kupitia ukurasa wao wa Twitter, Yanga wameandika kuwa wanajisikia furaha na wanaipongeza Azam kufanikisha kutwaa tena kombe hilo.

"Sisi Kama Mabingwa wa Kihistoria wa Ligi KUU Tanzania tunajisikia wenye furaha kutuma pongezi zetu za dhati kwa Mabingwa watetezi wa CECAFA Cup 2018, Azam FC kwa kutetea tena taji lao. PONGEZI!!!!!!"


7 COMMENTS:

 1. Na Azam itapowafunga vilevile washeherekee. Timu ya Simba iliyofungwa ni nusu Team B na kwa hayo yanga wayajue na wangoje katika innings

  ReplyDelete
 2. Yanga wasisahau kujipongeza kwa kuchomoa kucheza mashimdano ya Kagame.Msimu huu Yanga mtapata taabu sanaa

  ReplyDelete
 3. walijitoa wakiiogopa Simba....tena Simba yenyewe waliyoiogopa ni B. Ila kama Yanga ingeshiriki mashindano basi Simba wangeshusha kikosi kamili na hiyo ingesaidia kutwaa komme

  ReplyDelete
 4. Hahaaaaaaaa safi sana yanga pamoja na historia ya kuweka mpira kwapani😂😂😂

  ReplyDelete
 5. Duh!!!!Hawa jamaa watakua waliuza ile mechi ya mwisho ya ligi kuu walipofungwa na azam, kumbe wanajisikia furaha azam wakishinda, hahahahahah mapung'o fc

  ReplyDelete
 6. Duh!!!!Hawa jamaa watakua waliuza ile mechi ya mwisho ya ligi kuu walipofungwa na azam, kumbe wanajisikia furaha azam wakishinda, hahahahahah mapung'o fc

  ReplyDelete
 7. Yanga imebakia kufurahishwa na.ushindi wa wengine baada ya kuikimbia simba. Masikini roho zap

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV