July 22, 2018



Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Abbas Tarimba, ameanza kazi ya kulimaliza suala la hassan Kessy.

Tarimba ameanza mazungumzo na Kessy ikiwa ni siku chache baada ya kufanikisha suala la kumsajili tena Kelvin Yondani.

Yondani alionekana kutoelewana na uongozi wa Yanga kuhusiana na suala la maslahi yake.

Tarimba amethibitisha kuanza kazi ya kumalizana na Kessy baada ya kuwa amemsikiliza.

“Tulikutana na Kessy, tumemsikiliza na tunapanga kukutana naye mara ya pili ili kulifanikisha hili.

“Kama ilivyo kwa Yondani, tunaendelea kufanya juhudi ili kulimaliza suala hili la Kessy,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic