July 21, 2018


Kipa wa akiba wa Yanga, Beno Kalolanya, amefunguka juu ya kichapo ilichokipata timu hiyo katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia Yanga.

Yanga ilishindwa kutamba mbele ya Gor Mahia katika ardhi ya Kenya kwa kukubali kichapo cha mabao 4-0 jijini Nairobi kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza.

Kwa mujibu wa Radio One, Kalolanya ambaye amekuwa benchi kwa mrefu tangu asajiliwe na Yanga kutokana na uwepo wa Rostand, amesema wapinzani wao waliwazidi kwa kila kitu.

Kipa huyo ameeleza kuwa Gor Mahia walikuwa vizuri zaidi kwenye safu zote za ulinzi, kati na ushambuliaji hivyo kuepelekea Yanga kushindwa kuhimili mikiki-mikiki yao.

"Kiukweli kuwa tu mkweli wenzetu walituzidi kila kitu maana walikuwa bora kwenye kila idara ya uchezaji, walicheza mpira walivyotaka" alisema.

Baada ya kueleza hayo, Kakolanya ameeleza ana imani Kocha wake, Mkongomani, Mwinyi Zahera, atarekebisha mapungufu yaliyojitokeza ili kujiandaa na mchezo wa marejeano utakaopigwa jijini Dar es Salaam.

4 COMMENTS:

  1. Vipi arakibishe mambo na unambiwa kibali cha kufanya kazi hana na hakuna anayefuatilia. Sijui kama huyo Zaheara nae kaambulia chochote cha mshahara tangu kutuwa kwake

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yote anajua Mungu. Waliotaka Yanga iwe hivyo wanachekelea bila kuelewa Yanga ilikuwa pia ni mchango mkubwa wa mapato kwa serikali. Mwaka huu Yanga watapata shida ila nasema ukweli mwakani mambo ya Yanga yatarudi kama yalivyokuwa mwanzoni. Yanga ni taasisi kubwa haiwezi kupotea. Timu ya kihistoria Africa. Uko ufadhili wa ajabu umeandaliwa wa kuiinua Yanga kiuchumi na uwanja mkubwa utakaochukua watu zaidi ya 35 elfu utajengwa kwa ajili ya timu. Wenye macho hawaambiwi tazama. Hata kama Yanga itashuka daraja. Bado mambo ya Yanga yanaandaliwa kwa kasi kubwa. Team itawekwa kwa wawekezaji wa nje.

      Delete
    2. Hizi ndoto zako ni za alinacha za kuota mchana.Naona utaendelea kupata tabu sana.

      Delete
    3. wane kwanza kulipa mishahara

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic