July 21, 2018


Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wilaya ya Ubungo (UFA), Benjamini Mwakasonda, ameeleza namna Yanga ilivyosuasua na kuepelekea kupoteza kwa kipigo cha aibu mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Gor Mahia.

Akizungumza kupitia Radio One, Mwakasonda amesema tatizo kubwa la Yanga ilikuwa ni kuepeleka wachezaji wasio na uwezo wa kucheza dhidi ya Gor Mahia ambao walikuwa bora zaidi yao.


Mwakasonda ameeleza uzembe walioufanya viongozi wa Yanga ni kushindwa kumalizana na mabeki Hassan Kessy na kelvin Yondani mapema ili wakaweze kukipa kikosi nguvu kwenye mchezo huo.

Kiongozi huyo amefunguka akiamini Yanga ilikuwa ilikuwa butu katika sehemu zote za uchezaji na ndiyo maana ilipelekea kupoteza kirahisi mchezo huo uliokuwa muhimu kwa Yanga kupata matokeo.

Mbali na matokeo hayo, Mwakasonda amehoji pia juu ya uzembe mwingine wa Yanga kushindwa kufuatilia vibali vya Kocha wake, Mkongomani Mwinyi Zahera ambaye ana miezi sasa tangu atangazwe kusajiliwa.

Mwakasonda ameeleza kushangazwa na kitendo cha Zahera kuendelea kukaa jukwaa wakati ana muda mrefu sasa tangu ajiunge na mabingwa hao wa kihistoria katika Ligi Kuu Bara.

"Mimi nashangaa mpaka sasa Yanga haijakamilisha kupata vibali vya Kocha, ni jambo la kushangaza kuona Zahera tangu aje nchini mpaka sasa anakaa jukwaani" alisema.

3 COMMENTS:

  1. Yanga wapo kwenye kona hawawezi kufurukuta na huku wakisukumana bila yakujuwa namna ya kujiondoa. Jambo baya sana lililowavuruga wachezaji na wafuasi ni kutokana na na ahadi zisizo za kweli kila kukicha kuwa Manji anarudi kikosini na kuwa wameshamalizana na wachezaji katika mahitaji yote na kubainika baadae kuwa sikweli. Wanajivuruga wenyewe na na kuivuruga yimu na si hasha ukasikia wakati woeote Zaheri nae kaingia mitini kujiona anafanywa kama kinyago na inabidi watamke wazi kuwa Manji ametuwa zigo la madoriani yaliyokuwa yanamuumiza kichwa watangaze wazi ili kwaharaka wamtafute mwengine pindi wakimpata. Ni timu yangu na naumia sana.Wanawataka kina Yondani na huyo mdogo wake wasaini mkataba kwa mikono mitupu na wajikwamishe na huku timu nyengine zikiwataka kwa mamilioni mikononi

    ReplyDelete
  2. Sijaelewa vizuri Klabu ya Yanga ipo Jangwani Wilaya ya Ilala. Huyu Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wilaya ya Ubungo ameyasema hayo aliyoyasema kuhusu yanga kama maoni yake binafsi au kwa wadhifa alionao ndani ya Chama chake? Napenda tutofautishe nafasi zetu tunapotoa kauli ambazo zinaweza kutoa tafsiri za kuingiliana madaraka ya kazi. Au Yanga ipo Wilaya ya Ubungo kisoka?

    ReplyDelete
  3. Sifahamu, naomba nielekezwe kibali cha kufanya kazi nchini kinahitaji pesa au la na kama ni pesa ni kiasi gani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic