BODI YA LIGI YAJA NA UTARATIBU MPYA WA KUGAWA MAPATO YA MECHI ZA LIGI KUU BARA
Wakati Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) ikitarajia kutangaza ratiba ya mechi za Ligi Kuu Bara leo majira ya mchana, Mkurungezi wa Bodi hiyo, Boniface Wambura, amefunguka kuhusiana na mapato ya msimu ujao.
Wambura amesema katika msimu ujao wa Ligi Kuu, timu mwenyeji itakuwa inapewa fedha zote za mapato ya uwanjani tofauti na ilivyokuwa misimu ya nyuma kwa ngazi ya Ligi Kuu Bara.
Maamuzi hayo yamefikiwa kutokana na mapendekezo yaliyofanywa na klabu zenyewe pamoja na wadau wa soka hivyo sasa itakuwa tofauti na ilivyokuwa misimu mingine nyuma ambapo timu zote zilikuwa zikigawana huku mwenyeji akipata kiasi kikubwa tofauti na mgeni.
Mkurugenzi huyo amesema klabu na wadau ndiyo chachu ya kufanyika kwa mabadiliko hayo ya mapato ya mlango hivyo kuanzia sasa mgawanyo hautokuwepo tena kama ilivyokuwa imezoeleka.
Wambura ameeleza suala hilo atalifananua vizuri leo atakapokuwa ameitisha kikao na Waandishi wa Habari katika makao makuu ya Shirikisho hilo yaliyopo Karume, Ilala.
Enter your comment...nadhani ni utaratibu mzuri
ReplyDeletemimi naona nimpango wa kuzisaidia timu za mikoan ziinuka kiuchumi ingawa itakuwa na hasara kwa mgeni hasa simba na yanga zinapokuwa mikoan
Delete