CHAMBUA AELEZA MASHAKA YAKE JUU YA YANGA KUELEKEA MECHI VS GOR MAHIA LEO
Wakati Yanga ikitarajiwa kukipiga dhidi ya Gor Mahia FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika leo, mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Sekilojo Chambua, ameelezea mashaka yake kuelekea mtanange huo.
Chambua amesema anaamini kuwa mechi itakuwa ngumu akisema Yanga walifanya maandalizi ambayo ni tofauti na ukubwa wa mashindano.
Mchezaji huyo wa zamani ameeleza Yanga hawajajipanga vema kuelekea mechi hiyo kitu ambacho kinaweza kuwagharimu kulingana na timu ambayo wanaenda kucheza nayo kuwa imara.
Michuano ya KAGAME iliyomalizika wiki jana jijini Dar es Salaam imemfanya Chambua kuieleza kama ilikuwa nguzo ya kuwaimarisha zaidi Gor Mahia kutokana na upinzani wa timu ambazo walikutana nazo.
Aidha, Chambua amelishauri benchi la ufundi la Yanga kuhakikisha kuwa linatoa ushauri kwa wachezaji wake ili kuwapa nguvu na morali ya kufanya vizuri licha ya kikosi kuwa na changamoto kadhaa ikiwemo kukosekana kwa wachezaji stahiki.
Mlikuwa wapi kuwapa ushauri huu mapema? Saa hii msitake kuwavuruga wachezaji na benchi la ufundi wacheni wacheze naamini watashinda tuu.
ReplyDeleteKUNA KUNDI KUBWA LA WANACHAMA NA MASHABIKI WA YANGA WAMEPANGA KUFANYA TUKIO LA MASHAMBULIZI KWA WOTE WANAOHUSIKA NA KUIDHOOFISHA YANGA KWENYE USAJILI KUNDI HILO LITAFANYA VURUGU HIZO MUDA WOWOTE....WAMESIKIA MENGINE YA UCHUNGU IKIWAMO KOCHA MWINYI ZAHERA KUTOKUWA NA KIBALI MPAKA LEO HII, KELVIN YONDANI ANASAINI SIMBA JIONI HI I NA MENGINE....SASA USALAMA WA VIONGOZI WA YANGA MASHAKANI, AKIWAMO MANJI AMBAYE NAYE AMEGUNDULIKA KUWA KUSUASUA KWAKE KUINGILIA KATI KUNAWAWEKA WAO KATIKA SINTOFAHAMU...HABARI NDIYO HIYO!
ReplyDeleteLijipange tu Hilo kundi bado shishimbi
ReplyDelete