July 14, 2018


Na George Mganga

Kiungo aliyekuwa akiichezea Mtibwa Sugar ya Morogoro, Hassan Dilunga, amejiunga na mabingwa wapya wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 Simba SC kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.

Dilunga amezima ndoto za kuelekea Yanga kama ambavyo ilikuwa imeripotiwa awali akihusishwa kuelekea kwenye klabu hiyo yake ya zamani.

Awali kulikuwa na mvutano mkubwa baina ya viongozi wa Simba na Mtibwa juu ya usajili wa Dilunga ambapo Mtibwa walikuwa wanaonekana kumbania wakimuhitaji lakini pande zote mbili zimefikia makubaliano.

Simba sasa imeonesha nia ya kutaka kuimarisha zaidi safu yake ya kiungo kutokana na kuwa na wachezaji wengi kwenye safu hiyo akiwemo Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Said Ndemla na wengineo.

Usajili umefanikiwa ukielezwa ni pendekezo la Kocha Msaidizi, Masoud Djuma, kuomba aongezewe kiungo mwingine ili kukifanya kikosi cha Simba kuwa kipana zaidi kuelekea Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

8 COMMENTS:

 1. Tusije kujuta kwa mtindo huu wa kusajili kama vile ni kuandikisha watoto wa darasa la kwanza maana naona usajili mwingine ni kama vile tunaingizwa mkenge.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Dilunga mashine. Tunamuhitaji sana Simba. Sasa mambo yanazidi kunoga

   Delete
  2. Usiseme hivyo simba itakuwa na mashindano meng hivyo kilos kinatakiwa kiwe kipana na kuna mifumo ming sana pale msimbaz hivyo unaweza kukuta mchzaji anafit kwenye mfumo flan na huyu anafit akicheza mfumo huu xx soon kipya hapo sorry kama nimekukwaza lakn najua Niko sahihi.

   Delete
 2. Ajipange kupiga jazi, msimbazi sio pá mchezo mchezo

  ReplyDelete
 3. Kauli gani ya kimamluki ya kusema Simba usajili wa Dilunga ni kuingizwa mkenge? Hivyo kuna kiungo Bongo hivi sasa kama Dilunga? Dilunga angelikuwa mchezaji wa simba zamani sana kama si fitna za Bonafasi Mkwasa aliefanya figisu za kumpeleka yanga wakati yeye mwenyewe Dunga nia na mapenzi yake yalikuwa yapo simba na simba tayari walikuwa washamake move lakini wakati akiwa kocha wa Taifa Stars Mkwasa alitumia wadhifa wake kumpushi dilunga kwenda yanga. Na pengine wakati ule kama dilunga angefanikiwa kwenda Simba hivi sasa angelikuwa anafanya kazi ulaya au timu yeyote ya maana nje ya Tanzania ni kijana mwenye kujituma na kujua thamani ya kazi yake sema Yanga ilikaribia kuzima ndoto yake na alifanya busara kurudi mtibwa na nilishangaa sana kusikia eti anataka kurudi tena yanga. Yanga kwa sasa kazi yake kubwa ni kuua vipaji huo ndio ukweli.

  ReplyDelete
 4. dilunga karibu simba timu yenye amani achana na wambeya

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV