July 13, 2018


Chelsea inatarajiwa kuweka wazi uamuzi wake wa kutengana na Conte baada ya kuwatumikia kwa miaka miwili hivi karibuni.

Kufikia sasa, klabu hiyo imekataa kufunguka kuhusu hatma ya meneja huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 48 lakini inafahamika kwamba amefutwa kazi na hata wachezaji wa Chelsea wamekuwa wakimtakia heri na kumshukuru kwa muda aliokaa Chelsea..

Kwa mujibu wa BBC, Conte aliwasaidia kutwaa mataji ya ligi ya Premia msimu wake wa kwanza pamoja na Kombe la FA.

Licha ya Conte kuwaongoza wachezaji mazoezini wiki hii, hatma yake imekumbwa na taharuki huku mkufunzi wa zamani wa Napoli Maurizio Sarri akitarajiwa kujaza pengo lake.

The Blues wa Chelsea tayari wamefikia makubaliano ya kuwasili kwa Sarri mwenye umri wa miaka 59.

Iwapo usajili wa Sarri utadhibitishwa, atakuwa mkufunzi wa tisa wa Chelsea tangu Mrusi Roman Abramovich aliponunua timu hiyo 2003.

Licha ya kutoinua taji lolote na Napoli miaka mitatu aliyowaongoza, Sarri amerudisha hadhi ya Napoli na kuwawezesha kumaliza nafasi ya pili, tatu, na pili nyuma ya Juventus msimu uliomalizika wa 2017-18.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic