AZAM YAAMUA KUMTUMIA CHILUNDA KAGAME LEO KAMA TISHIO KWA SIMBA
Uongozi wa klabu ya Azam FC kupitia kwa Ofisa Habari wake, Jafaar Idd Maganga, umesema utamtumia mchezaji wake, mshambuliaji, Shaban Idd Chilunda katika mchezo wa fainali ya KAGAME dhidi ya Simba SC.
Maganga ameeleza Azam walifikia uamuzi huo ili kukipa kikosi chao nguvu ya kukabiliana na Simba kutokana na mchango wa Chilunda ambaye ameonekana kuwa kwenye kiwango kizuri hivi karibuni.
Ikumbukwe Azam wamemalizana na klabu ya CD Tenerife anayochezea Faridi Mussa nchini Hispania na alitakiwa kuelekea huko lakini Azam wameongea na viongozi wa timu hiyo ambayo anapaswa kwenda kwa mkopo wakiomba atumike katika mchezo wa leo.
Baada ya kuandika barua hiyo, Chilunda sasa rasmi atakuwa sehemu ya mchezo wa kesho dhidi ya Simba utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam majira ya saa 12 jioni.
Azam walifuzu kutinga hatua hiyo kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya miamba wa Kenya, Gor Mahia FC huku Simba wakiifunga JKU kutoka visiwani Zanzibar kwa bao 1-0.
Yupo anayeweza kumtisha mnyama Simba, ambapo anaponguruma kila mnyama pori anatafuta pakujificha
ReplyDeleteSielewi sheria za mchezaji wa mkopo anakuwa vipi? Lakini ninachoelewa mimi chilunda bado mchezaji halali wa Azam mpaka atakapo anza kuitumikia Tenerife.Na kama Azam wanakubali kupewa masharti kwa mchezaji wao wenyewe na klabu inayotaka kumuazima huo ni ubwege. Ni vizuri kuwapa wachezaji nafasi kujitangaza nje lakini tusiewe walaini mno kwani huyu kijana angepiga tu daraja la pili au hata la tatu pale belgum na muda si mrefu angetoka.
ReplyDeleteAcheze Chilunda acheze Zayd na waongezeke wengine waje. Simba itashinda tuu
ReplyDelete