CHELSEA YATAJA KUWANASA NYOTA WAWILI: TETESI KUBWA ZA SOKA BARANI ULAYA LEO ALHAMIS
Meneja mpya wa Chelsea Maurizio Sarri angependa kuwasaini wachezaji wawili wa Juventus - raia wa Argentina Gonzalo Higuain, 30, na raia wa Italia Daniele Rugani, 23 - lakini hata hivyo hawezi kuwasaini wachezaji kadhaa wa Napoli ambao angependa kuwasaini. (Evening Standard journalist Tom Collomosse kwenye BBC Radio 5 live)
Liverpool wamewapiku Chelsea katika kumsaini kipa wa Roma raia wa Brazil Alisson, 25, na wanatarajiwa kuthibitisha mkataba huo wa thamani ya pauni milioni 66.8 kabla ya wikendi. (Liverpool Echo)
Manchester United wanatathmini kuwinda wachezaji wawili wa Bayern Munich - mshambuliaji raia wa Poland Robert Lewandowski, 29, na kiungo wa kati mhispania Thiago Alcantara, 27 - huku naye beki mbelgiji Toby Alderweireld, 29 akilengwa. (Independent)
Usain Bolt anakaribia kajiunga na ligi ya Australia
Alcantara anataka kurudi Barcelona, miaka mitano baada ya kuhamia Bayern Munich. Mhispania huyo ameshinda mataji matano ya Bundesliga katika misimu mitano akiwa Bayern. (AS)
Beki wa Manchester United raia wa Italia Matteo Darmian, 28, anakaribia kuhamia Juventus baada ya miaka mitatu huko Old Trafford. (Football Italia)
Fulham wanakaribia kuthibitisha mkataba wa thamani ya pauni milioni 20 kwa mshambuliaji wa Newcastle mwenye miaka 23 raia wa Serbia Aleksandar Mitrovic, ambaye alifunga mabao 12 wakati akicheza kwa mkopo kuwasaidia kuingia ligi ya primia. (London Evening Standard)
Tottenham wako kwenye mazungumzo na Aston Villa kuhusu kiungo wa kati wa England Jack Grealish 22, ambaye amewekewa thamani ya kati ya pauni milioni 30 na 40 na klabu hiyo. (Sky Sports)
Burnley wamefanya mazungumzo na Swansea City kuwataka kuwasaini wachezaji wawili walio na thamani ya pauni milioni 20, mlinzi raia wa England Alfie Mawson, 24, na kiungo wa kati ambaye pia ni raia wa England Sam Clucas, 27. (Mail)
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment