July 19, 2018


Baada ya dhahama ya kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Gor Mahia FC iliyokipata Yanga jana jijini Nairobi, Kenya kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, Mjumbe wa Baraza la Wazee wa klabu hiyo, Ibrahim Akilimali, ameibuka na kauli ya kutisha.

Akilimali ameutaka uongozi wa Yanga kuhakikisha ina wafukuza wachezaji wote katika kikosi hicho akiamini wamekosa mchango wa kuisaidia timu na badala yake abaki Yondani peke yake.

Mzee huyo amesema matokeo ya jana yanazidi kuleta taswira mbaya katika timu hiyo na namna mwenendo mzima wa klabu unavyoenda hivi sasa hivyo ameona ni wakati mwafaka kwa wachezaji wa Yanga kupigwa panga.

Kauli ya Akilimali imekuja kufuatia matokeo ya jana ya kipigo cha mabao manne ambayo yamesababisha Yanga kujiwekeza mazingira magumu zaidi kusonga mbele kuelekea hatua inayofuata.

Aidha, Akilimali ameutaka pia uongozi wa Yanga kuitisha uchaguzi ili kupata watawla wapya watakaofanya kazi kwa ueledi mkubwa ili kuisaidia timu hiyo kuimarika ili kurejesha makali yake kama ya mwanzo.

Akilimali amesema inabidi Yanga waitishe uchaguzi mpya haraka ili kupata viongozi wapya waweze kuikwamua klabu kutoka kwenye hali ya ukata wa fedha uliopo hivi sasa iweze kujiimarisha kiuchumi.

Kauli hiyo imekuwa ya mwendelezo kwa Akilimali ambapo mara nyingi amekuwa akishauri uchaguzi ufanyike ili kumpata mbadala wa Yusuf Manji ambaye alijiuzulu wadhifa huo.

16 COMMENTS:

  1. moja ya mambo yananikera katika media za kitanzania ni kumpa mileage huyu mzee!!! wa nini???

    ReplyDelete
  2. Huyu mzee anatakiwa kutopewa nafasi kabisaaaaaa. Hata falinali ya kombe la dunia kuna mtu alikula nne alafu kama hakuna motivation performance inatoka wapi. Tuangalie kwanza masilahi ya wachezaji wetu, tumefukuza wengi kama Dilunga, Zhahir, banuhuzi na leo tunata kuwanunua tena kwa kugombania. Tucheze na kuuongoza mpira UCHAWI HUU NI MBAYA KABISAAA

    ReplyDelete
  3. Mawazo ya Mzee akilimali sio ya kubeza,huyu Mzee huwa anaona mbali sana japo kwa hilo la kufukuza wachezaji wote amebugi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kaka heshima kwa wazee wetu ni jambo la msingi sana kwa sababu ni vizuri kupata maoni yao wakiwa bado wako na uwezo wa kufanya hviyo. NAKUOMBA UNISHAURI AMA KUNIKUMBUSHA ni lini ameona mbali kwa mfano ulio sahii. Wabakie kuwa WATOA USHAURI lakini wasiwe watu wa kutoa MAAMUZI maana wakati wao umepita ukweli ndio huo ni sehemu tu ya michango ya mawazo yao inahitajika na si kitu kingine.
      KUWA NA JICHO LA MBALI UTANGUNDUA TUTAPATA TAABU SANA kama tutakaribisha mfumo wa kila mtu kuiingilia maamuzi ya uongozi na hata KUONGEA na watu wa Yanga

      Delete
  4. wewe muandishi wa hii habari ni MSENGE SANA, habari hii uliwahi kuiandika kama ilivyo wakati Yanga ilipocheza na USM alger na kupoteza kwa magoli ma 4 ukasema AKILIMALI MME WA MAMA YAKO, Amesema YONDANI ndio mchezaji anayetakiwa kubaki yanga, kwa hiyo ulichifanya ni kuicopy kama ilivyo ukaedit sehemu ya JINA la timu na NCHI, kwa watu wasiofatilia Hii blog wanajua hii ni taarifa mpya wakati sio, ila ni ushenzi wako wa kuedit taarifa zilizopita kwa kuwa unaona bila kuandika habari za yanga hakuna atakayesoma blog yenu...inaonekana unafurahia sana hali inayoendelea NDANI ya club ya yanga na ndio maana kila siku ukitaka kuwavuruga wanaYANGA basi lazima umuandike huyu MUME WA MAMA YAKO.

    ReplyDelete
  5. HUYO UNAYETAKA ABAKI SI NDO ALIGOMA KUSAFIRI NA TIMU?

    ReplyDelete
  6. Sasa broo ulitaka aandike yanga yamsajili messi au ronaldo ndio uamini.
    Kiuhalisia yamga ina hali mbaya viongozi wake hawana hadhi ya kuongoza klabu na wamefeli na wanagoma kuitisha uchaguzi kuziba nafasi zilizo wazi na ni agizo la serikali.
    Amekosea kumpa nafasi akilimali lakini hata yanga kuna matatizo zaidi ya nafasi anayopewa akilimali na media.
    Piganeni kuikomboa timu kutoka hapo ilipo na si kushindana na wanaowaambia ukweli.

    ReplyDelete
  7. Sasa broo ulitaka aandike yanga yamsajili messi au ronaldo ndio uamini.
    Kiuhalisia yamga ina hali mbaya viongozi wake hawana hadhi ya kuongoza klabu na wamefeli na wanagoma kuitisha uchaguzi kuziba nafasi zilizo wazi na ni agizo la serikali.
    Amekosea kumpa nafasi akilimali lakini hata yanga kuna matatizo zaidi ya nafasi anayopewa akilimali na media.
    Piganeni kuikomboa timu kutoka hapo ilipo na si kushindana na wanaowaambia ukweli.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wana Yanga wenzangu turudi kwenye hoja tusichanganye mambo hapa kila siku tunaendelea kukosea. HAPA TUNAJADILI JUU YA AKILI NI MALI NA KAULI ZAKE AMBAZO NDIO HOJA YA MSINGI HATUzuNGUMZII UCHAGUZI. KWA TAARIFA TU ILI YANGA IFANYE VIZURI LAZIMA IWE NA MSEMAJI MMOJA TU. Kama kuna wakati yanga ilikuwa inafanya vizuri ni wakati ule mzee wetu alikataliwa na mwenyekiti kuongea ongea hovyo. Hata akija kiongozi gani kwa mfumo uliopo hatoweza kuongoza maana kiongozi yapaswa awe mmoja na wasaaidizi wake tu

      Delete
  8. Unaweza itisha uchaguzi alafu WANAJANGWANI wakawarudisha hao unawaona hawafai labda kama umeanza Campain. ALAFU HAIWEZEKANI MTU AENDESHE TAASIS KUBWA KAMA URAIANI ALAFU ASHINDWE KUONGOZA YANGA. HAKUNA MIUJIZA HAPA LAZIMA TUKINYEE HICHI KIKOMBE NA KUTAFUTA UTATUZI WA KUDUMU KWA KUHESHIMU MAWAZO ya wanachama wote

    ReplyDelete
  9. Mi nafikiri kwa sasa wana Yanga si wakati wa kulumbana cha msingi tuangalie hoja hapa ni nini? Kipubwa kufanya kila linalowezekana ili kuikomboa timu, matusi, kashfa na kejeli hazitachangia kuondoa Yanga ilipo. Bao nne ni nyingi na tusifanyie mchezo. Kufungwa kwa Yanga iwe njia ya kuona pale ambapo palikosewa hata kikosi kilipangwa vibaya Haji Mwinyi kucheza kiungo na wale watoto kuanza mwanzo, siyo sahihi ona dakika chache za Amis Tambwe uliona alivyoonyesha ukubwa ni dawa, kwa nini Pato Ngonyani na Juma Makapu hawakupangwa mwanzoni? Hebu tuanzie hapo, Kumjadili mzee Akilimali ni kupoteza muda. Aongee maneno yakiisha atanyamaza. Hata Simba kuna Kilomoni wamempuuza na sasa haongei kitu.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakubaliana na wewe kabisa ila kufungwa ni sehem ya mchezo japo inauma. Timu zote hufungwa tena zaidi ya goli hizo kikubwa hapa ni kwa nn tumefungwa kwa aibu kubwa hivi

      Delete
  10. Mwisho wa yote mpira pesa story zilipendwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic