July 17, 2018


Kikosi cha Yanga kinafanya maandalizi ya mwisho leo kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC utakaopigwa kesho jijini Nairobi, Kenya.

Yanga inaenda kucheza mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu za kwenda suluhu tasa ya 0-0 dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda ambayo wapo nayo kundi moja (Kundi D), mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi ya keshio itawapasa Yanga kuhakikisha wanapata ushindi kujiwekea mazingira ya kusalia kwenye michuano hiyo ambapo hivi sasa bado wana alama moja pekee katika msimamo wa kundi hilo.

Ikumbukwe Yanga ilipoteza dhidi ya MC Alger kwenye kibarua cha kwanza pia suluhu dhidi ya Rayon na kuwafanya kuwa kwenye mazingira magumu kunako kundi D.

Dawa pekee ya Yanga kujipa matumanini ni kuhakikisha inawafunga Gor Mahia kesho kisha kuanza maandalizi mengine ya mchezo wa mkondo wa pili utakaopigwa Dar es Salaam.

Yanga itashuka dimbani bila wachezaji wake mabeki Hassan Kessy na Yondani ambao imeelezwa wamebaki Dar es Salaam wakihitaji kuongezewa mikataba mipya.

2 COMMENTS:

  1. KUNA KUNDI KUBWA LA WANACHAMA NA MASHABIKI WA YANGA WAMEPANGA KUFANYA TUKIO LA MASHAMBULIZI KWA WOTE WANAOHUSIKA NA KUIDHOOFISHA YANGA KWENYE USAJILI KUNDI HILO LITAFANTA VURUGU HIZO MUDA WOWOTE....WAMESIKIA MENGINE YA UCHUNGU IKIWAMO KOCHA MWINYI ZAHERA KUTOKUWA NA KIBALI MPAKA LEO HII, KELVIN YONDANI ANASAINI SIMBA JIONI HI I NA MENGINE....SASA USALAMA WA VIONGOZI WA YANGA MASHAKANI, AKIWAMO MANJI AMBAYE NAYE AMEGUNDULIKA KUWA KUSUASUA KWAKE KUINGILIA KATI KUNAWAWEKA WAO KATIKA SINTOFAHAMU...HABARI NDIYO HIYO!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hizo taarifa za kutolewa taarifa kwa vyombo vya usalama ili kuzuia hali yoyote mbaya inayoweza kutokea kutokana na mipango hiyo

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic