KILIMANJARO QUEENS YAWASILI SALAMA KIGALI TAYARI KWA CECAFA
Timu ya Wanawake ya Tanzania Bara “Kilimanjaro Queens” imefika salama Kigali, Rwanda leo asubuhi.
Kilimajaro Queens imewasili nchini humo kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya CECAFA kwa Wanawake yanayoanza Julai 19 2018.
Kikosi hicho kimeamua kuwasili mapema ili kutowapa uchovu wachezaji wake na kuzoea mazingira ikiwemo hali ya hewa huko Rwanda.
Benchi la ufundi limesema maandalizi kuelekea mashindano hayo tayari yameshakamilika ambapo sasa wanasubiri siku ifike kwa ajili ya kuanza mechi za michuano.
0 COMMENTS:
Post a Comment