July 19, 2018


Hali imezidi kuwa si shwari kunako klabu ya Yanga ambapo imeripotiwa kuwa Katibu Mkuu Charles Boniface Mkwasa ameandika barua ya kuomba kujiuzulu wadhifa wake.

Hatua ya Mkwasa kufanya maamuzi hayo imetokana na kusumbuliwa na matatizo ya kiafya kiasi cha kwamba imesababisha ashindwe kutekeleza majukumu yake ya kazi kwa ufasaha.

Imeleezwa kuwa barua hiyo imesema Mkwasa ameomba kupumzika kutokana na hali yake kiafya kuwa si rafiki na kazi anazopaswa kuifanyia Yanga hivyo ameona ni vema akakaa pembeni.

Mkwasa ambaye aliwahi kuichezea Yanga miaka ya nyuma ameanza kusumbuliwa na afya yake baada ya kuchaguliwa kuchukua wadhifa wa Ukatibu Mkuu miaka miwili nyuma wakati Yusuph Manji akiwa Mwenyekiti wa klabu.

Mbali na kuichezea Yanga, Mkwasa alichaguliwa kuwa Kocha Msaidizi wa Yanga akiwa chini ya Mholanzi, Hans van der Plujim ambaye alitimkia Singida United na sasa Azam FC.

Tukio hilo limetokea ikikumbukwa hivi karibuni aliyekuwa mmoja wa wajumbe wa utendaji katika klabu hiyo, Salum Mkemi, naye kuandika barua ya kujiuzulu kwasababu za kutoendana sawia na matakwa ya wanachama.


3 COMMENTS:

  1. Hivi Mkwasa anajiuzuru au anaacha kazi? ?

    ReplyDelete
  2. Mpira ni biashara, club znapaswa kuendeshwa kama taasisi, iajiri watu wenye taaluma Kwenye kila position ya utawala
    Alipofikia Pana tosha kwa uwezo wake ameifikisha yanga hapo ilipo

    ReplyDelete
  3. Mkwasa na Manji wanaelewana. Maadam Manji tulikataa asijiuzuru vema na Mkwasa abakie madarakani wasimamie mabadiliko makubwa ya mfumo wa uendeshaji klabu yetu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic