July 19, 2018


Baada ya kupokea kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Gor Mahia FC jana katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika, mashabiki wa Yanga wameutaka uongozi kukisafisha kikosi upya.

Hatua hiyo imekuja kufuatia kipigo hicho cha aibu ugenini wakieleza kutoridhishwa na aina ya wachezaji wengi ilionao wakidai kuwa hawaendani na ukubwa wa kikosi cha Yanga.

Baadhi wametupa lawama zao nyingi kwa kipa Mcameroon, Youthe Rostand, ambaye wamemuelezea kuwa amekuwa mzigo zaidi kwa sasa na hii ilianza tangu raundi ya pili ya Ligi Kuu Bara msimu uliopita wakisema inabidi aondoke.

Goli nne alizofungwa Rostand leo, kupitia mitandaoni na hata katika mitaa mbalimbali vijiweni, wengi wamekuwa wakihoji juu ya ubora wa kipa huyo na wengine wakiitupia lawama safu ya ulinzi na ushambuliaji.

Tangu kuondoka kwa Kocha Mzambia, George Lwandamina, Yanga imekuwa ikiendelea na rekodi mbovu kutokana na kukosa matokeo chanya badala yake kikosi kimekuwa hakifanyi vema kama zamani.

6 COMMENTS:

  1. SISHANGAI NILIWAHI KUSEMA HUKO NYUMA BENCHI LOTE LA UFUNDI, WACHEZAJI, VIONGOZI NA SYSTEM NZIMA YA YANGA NI MBOVU.....KOCHA HUYU AKIENDELEA HIVI ATAIRUDISHA TIMU NYUMA KABISA LAZIMA MKATABA UVUNJWE HARAKA SANA....NA BENCHI LOTE LA UFUNDI. KWELI KUNA SHIDA YA PESA LAKINI HATA UFUNDI UONEKANE....MCHEZAJI ANAYECHEZA NAMBA 3 LEO ANAPANGWA NAMBA 6. HALAFU NILISEMA KUWA SIO LAZIMA KUSHIRIKI MASHINDANO YA CAF KAMA WACHEZAJI, TIMU KWA UJUMLA HAIANDALIWI, POSHO HAKUNA, MOTISHA HAKUNA, SIO LAZIMA KUSHIRIKI....AU KAMA VIPI MKOPE FEDHA BENKI MUIANDAE TIMU. PIA KUNA MAADUI WAMEPEWA AU WAMEPENYEZWA KLABUNI....ILI KUIDHOOFISHA KLABU INAANZIA KWA WAFADHILI WA YANGA (WANAOJITOLEA KUIFADHILI), TFF, THEN KWENYE UONGOZI WA KLABU, WACHEZAJI MPAKA BENCHI LOTE LA UFUNDI.....HAPA HAWA MAADUI WASIFIKIRI AIBU NI YA YANGA TU....HAPANA NI AIBU YA TAIFA..

    ReplyDelete
  2. Kwani kipa bila beki imara atalindaje lango? Acheni lawama kwa Youthe Rostand jamani, kwa kweli kikosi kile hakikustahili kucheza na Gor Mahia, mbona Tshishimbi alipambana? Hakuna jitihada za makusudi za wachezaji kutokana na mfumo wa mchezo wenyewe.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  3. Timu mbavu dhaifu kabsa, hata ikicheza ndondo cup haipatkn matokeo
    Inashangaza viongozi gn hawatumii uwezo WA kufikir kuendesha club, kuna changamoto ya pesa wanashindwa kuchukua mkopo, kulipia madeni ya wachezaj kuongeza molari wafanye vizuri wapate pesa ya mrejesho, club ni taasisi yenye assets za kuweza kukopesheka na banks, watu wanabid wawe serious na michezo, timu za ndani hazina mipango serikali haichukui hatua kwann club zisizo na mipango zichukuliwe hatua? Taifa linatiwa asbh, kwa mifumo hii kushiriki afcon au world Cup yesu atatukuta tunaishia Kwenye hatua ya kufuzu

    ReplyDelete
  4. Maafa ya Jangwani girls yameendelea huko Kenya. Wamepata division four, watapata tabu sana mwaka huu.

    ReplyDelete
  5. Jamani unaposema wachukue mikopo, kwamba klabu ina asset; ebu sema asset zilizopo Yanga kuifanya ikopesheke bila kuwa na tashwishwi yeyote? Ina wanachama ndio, je hao wanachama wanashindwaje kulipa mishahara ya wachezaji walau kwa miezi sita ya mbele? Ukweli ni kwamba hakuna lolote kwenye wanachama bli ni wapiga kelele tu! Unadhani benki wanakopesha kwa mali kauli? Labda sio benki za kipindi hiki cha awamu ngumu ya Tano. Klabu haina kiwanja cha kuweka dhamana wataweka dhamana lile ghorofa la kizamani kwa mkopo wa shilingi ngapi? Halafu kuna kipindi mnasema eti Yanga ni klabu ya wanainchi mkimanisha pia eti mna mtaji wa vigogo wa serikali wanaoweza kubusti mambo, sasa lawama kwa kiongozi wa Yanga zinakujaje wakati na yeye ni kama mwananchi wa kawaida tu? Hivi ukiwa mbunge mana yake unaweza kujenga barabara ya lami au kujenga barabara za jimbo lako kwa hela yako mwenyewe mfukoni. Acheni LAWAMA.

    ReplyDelete
  6. Timu dhaifu kabisa hta huyu kocha mpya hafai kabisa hatairudisha timu nyuma timu wapewe wazawa wa hapa hapa na yule golikipa hafai kabisa takribani wachezaji 13 WA kuachwa kabisa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic