July 17, 2018



Unaweza ukasema kweli sasa Jeshi la Polisi limenuia kuendeza michezo nchini.

Maana Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro, leo amefungua kambi ya wanamichezo wa polisi wanaojiandaa kushiriki Michezo ya Shirikisho la Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (EAPCCO GAMES 2018) inayotarajiwa kuanza mwezi ujao hapa nchini.

Kambi hiyo ambayo ina zaidi ya wanamichezo 200 ambao wanatarajiwa kushiriki michezo mbalimbali kwenye mashindano hayo ikiwemo soka, mpira wa mikono, volleyball, netiboli, ngumi, taekwondo, karate na kulenga shabaha, ipo katika Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Dar.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo uliofanyika katika chuo hicho, IGP Sirro amewataka wanamichezo hao kulinda heshima ya nchi kwa kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.

“Nawaomba mjiandae vizuri kuhakikisha mnaileta heshima nchi na jeshi la polisi kwa jumla. Inaeleweka kwamba kuna zaidi ya polisi elfu arobaini na tano, lakini ninyi ndiyo mmechaguliwa kutuwakilisha, hivyo kafanyeni kweli.

“Hivi karibuni tu nilipoenda Uganda kwenye mkutano wa wakuu wa polisi, kila nchi ilikuwa inatamba itafanya kweli hivyo basi ili kudhihirisha sisi tupo vizuri, tunataka ushindi ubaki hapa nyumbani,” alisema IGP Sirro.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic