July 17, 2018


Na George Mganga

Baada ya CECAFA kuipiga rungu klabu ya Gor Mahia FC kushiriki michuano ya KAGAME kwa miaka miwili huku likimtaja kocha wake, Dylan Kerr, kuwa alikuwa akitukana matusi, Kerr ameibuka na kukanusha suala hilo.

Mapema baada ya michuano hiyo kumalizika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam kwa Azam FC kufanikiwa kutwaa ubingwa mbele ya Simba, CECAFA waliamua kuifungia Gor Mahia miaka hiyo baada ya kugomea medali pamoja na kocha wake kutukana matusi kwa wamuzi,

Baada ya hukumu hiyo, Kerr amewajibu CECAFA kwa kusema si kweli na akieleza kama alikuwa akifanya hivyo imekuwaje hakutolewa nje ya Uwanja na Waamuzi?

Aidha, ameeleza kuwa pale Kocha inapotokea anashindwa kuonesha ustaraabu wakati mchezo unapoendelea anapaswa kuondolewa haraka Uwanjani na Mwamuzi kwasababu atakuwa anaenda kinyume na taratibu za mchezo husika.

"Sikutolewa nje ya Uwanja katika mchezo wowote ule, sijajua kwanini CECAFA wameamua kufanya hivyo na kunilalamikia kuwa nimewatukana Waamuzi. Napingana na uamuzi wao kwkauwa sikufanya kitu kama hicho" alisema Kerr.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic