WAKATI SIMBA IKIENDELEA NA USAJILI, BEKI WAKE KIRAKA ANUKIA MWADUI FC
Wakati kikosi cha Simba kikiendelea usajili wa nyota wapya kwa ajili ya kuiboresha timu kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara, imeelezwa Mwadui FC wameanza kumyatia beki wake Ally Shomari.
Taarifa kutoka Shinyanga zinaeleza mabosi wa Mwadui tayari wameshaanza harakati za kuwania saini ya beki huyo ambaye hakuwa sehemu ya kikosi cha kwanza ndani ya Simba katika msimu uliopita.
Mwadui wameanza mazungumzo na uongozi wa Simba ili kuwapatia Shomari kwa mkopo kwa ajili ya kuisaidia timu hiyo ambayo haikufanya vizuri msimu wa 2017/18.
Shomari ana uwezo wa kucheza beki namba 2, 3, 4 mpaka 5 pia ana uwezo wa kupanda mbele kucheza namba 7.
Ikumbukwe Shomari alisajiliwa na Simba akitokea Mtibwa Sugar kabla ya msimu wa 2017/18 kuanza na hakuweza kutumika zaidi kwenye mechi lukuki za msimu uliomalizika ambao Simba wamejitwalia ubingwa wa Ligi Kuu.
0 COMMENTS:
Post a Comment