July 21, 2018


Safari ya kinda wa Azam FC, Shaban Chilunda bado haijakamilika kutokana na viongozi wa Klabu ya CD Tenerife ya Hispania kuendelea kushughulikia kibali cha nyota huyo kuweza kufanya kazi nchini humo.

Tenerife imeingia mkataba wa miaka miwili na nyota huyo aliyeibuka mfungaji bora wa michuano ya Kagame iliyomalizika hivi karibuni baada ya kutupia kambani mara nane na kuipa taji la ubingwa Azam.

“Kwa sasa klabu yangu mpya inshughulikia kibali cha mimi kuweza kufanya kazi Hispania na taratibu zote zikikamilika ndipo nitakuwa na uwezo wa kuondoka hapa na kwenda kuanza kazi sababu wenzetu wanazingatia sheria sana.

“Sababu huwezi kwenda kule kama huna kibali cha kazi kila kitu kikikamilika ndipo nitaweza kupewa visa na kuondoka hapa nchini kwa ajili ya kuanza kazi yangu rasmi ndani ya Tenerife,” alisema Chilunda ambaye ameweka rekodi Kagame. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic