July 19, 2018


Kiungo Mshambuliaji wa klabu ya Juventus, Paulo Dybala, amempiga dongo moja la hatari Muargentina mwenzake, Lionel Messi juu ya ujio wa Cristiano Ronaldo ndani ya klabu hiyo.

Dybala ambaye imekuwa ikielezwa hana ukaribu na Messi amesema ujio wa Ronaldo ndani ya Juventus utamfanya acheze kwa maelewano mazuri zaidi akiwa sambamba naye.

Kiungo huyo ameeleza kuwa ni wakati mwafaka sasa wa kumuonesha Messi pamoja na Gonzalo Higuain namna gani ya kucheza na Ronaldo baada ya kukosa nafasi kwenye michuano ya Kombe la Dunia Urusi.

Dybala amefikia maamuzi ya kusema hayo baada ya kushindwa kupata nafasi wakati akiwa Urusi na kikosi cha timu ya taifa ya Argentina ambapo Messi na Higuain walipata nafasi ya kuanza huku yeye akikaa benchi.

Katika michuano hiyo iliyomalizika siku kadhaa zilizopita, Argentina iliishia hatua ya makundi kwa kichapo cha mabao 4-3 dhidi ya Ufaransa na kuondolewa rasmi kuendelea na michuano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic